Hamis Kitambi anahitaji msaada wetu…

Hamisi Kitambi ni mmoja wa wanamuziki wakongwe na hazinakubwa iliobakia hapa nchini Tanzania ,bwana Hamisi Kitambi mtunzi wa nyimbo nyingi , mojawapo ya nyimbo zake ni ule wimbo mzuri maarufu kwa jina ” Mpenzi wangu mwenye rangi ya Chungwa” kwa wale wenye kumbukumbu wanajua radha ya utamu wa wimbo huo.

kitambis

Mkongwe huyu Hamisi Kitambi amefanya kazi na bendi nyingi zikiwamo Tabora jazz,Unyanyembe band,  KIKO KIDS, Dar-es-salam JazzBand, Western Jazz. Hadi anapata ajali ya gari alikuwa Juwata (OTTU) Jazz sasa Msondo Ngoma aka Baba ya Muziki. Mwanamziki huyu mkongwe Hamisi Kitambi alipata ajali akiwa katika gari yeye na wanamziki wenzie wa  Msondo Ngoma, walipokuwa safarini Tanga!.Mzee Hamisi Kitambi kama anavyoonekana pichani,miguu yote imevunjika na amewekewa vyuma,cha kusikitisha zaidi ni kuwa, tangu apate ajali ndio katupwa tii! ,Huduma muhimu hana, mtaji wa masikini ni MIGUU YAKE nayo ndio kama anavyoonekana.

kitambiddd

Tujaribu kumsaidia mzee wetu huyu mwanamuziki mkongwe Hamisi Kitambi anapatikana  kwa simu hii Dar 0713576475.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments