Timu nane zawasili Dar kwa michuano ya netiboli

TIMU za mataifa nane zimewasili nchini tayari kwa mashindano ya kimataifa ya netiboli ya ‘Inter Nations Netball Tounament’, yatakayoanza kesho kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mashindano hayo ambayo yanashirikisha nchi 10 kutoka Afrika Tanzania imepangwa kuvaana na Lesotho katika mchezo wa Ufunguzi kesho.

Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Bayi alisema timu hizo zitafikia katika Hotel ya Blue Pearl na Land Mark zilizopo Ubungo ambapo wachezaji na viongozi wao watakaa.

Alisema maandalizi kwa asilimia kubwa yamekamilika na timu ipo katika hali nzuri kimchezo na kiafya na kuahidi kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Nchi zilizowasili ni pamoja na Afrika Kusini,Zimbabwe pamoja na Swazland. Tanzania imepangwa kundi A na nchi za Namibia,Zimbabwe na Afrika kusini.

Kundi B zipo nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Zambia na Swaziland ambapo pazia litafunguliwa kati ya Malawi na Kenya.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments