Uhaba wa vitanda waikumba Afrika Kusini Kombe la Dunia RUSTENBURG, Afrika Kusini

JIMBO la North West linakabiliwa na upungufu wa vitanda 4 000, na vyumba vya mtu mmoja mmoja tayari kwa Fainali za Kombe la Dunia 2010.

Waziri wa Maendeleo ya Uchumi na Utalii, Mmaphefo Matsemela, alisema wiki hii kuwa katika eneo hilo, kuna vitanda 18 000 tu na bado vinahitajika vitanda zaidi ya 22 000.

Kwa ujumla vitanda 1,400 bado vinahitajika katika hoteli za nyota moja, wakati vitanda 4,300 katika mahoteli ya nyota mbili, ambazo nyingi hutoa huduma ya kulala na kifungua kinywa pekee.

Katika hoteli za nyota tatu, ikiwemo nyumba za wageni, loji zinahitaji vitanda zaidi ya 12,100 na vitanda 4,200 vinahitajika katika hoteli na nyumba za wageni zenye hadhi ya nyota tano.

“Kuna vitanda 18 000 katika jimbo zima, na tunatoa wito wahusika kusaidia katika hili ili tuweze kujipanga kufanikisha fainali,” alisema Matsemela.

Mpango uliopo kwa sasa ni kutengeneza makazi ya muda ikiwemo ujenzi wa mahema na kuwataka wahusika wa masuala ya malazi kuhakikisha wanaboresha huduma ya malazi kipindi chote cha fainali za Kombe la Dunia.

“Hii ni changamoto na kuna timu nne zitakuwa hapa pamoja na mashabiki wao, sasa kuna haja ya kujiandaa kwa kujipanga mapema,” alisema mwanamama huyo.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments