TFF na Yanga juu ya George Owino

Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) limeitaka timu ya Yanga kukata jina moja la mchezaji wake mpya wa kigeni ili kumpisha mlinzi wake toka Kenya George Owino.

Yanga imesajili wachezaji kumi wa kigeni na katika hao Owino hayupo ila Yanga hawakutangaza kumuacha na mkataba wake haujaisha hivyo TFF imesema bado inamtambua kuwa ni mchezaji halali wa timu hiyo ya Jangwani.

Katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema uamuzi huo umechukuliwa na kamati ya mashindano ambayo imegundua kasoro hizo kwenye usajili wa timu ya Yanga.

Wachezaji wapya wa wakigeni ambao wamesajiliwa na YANGA kwaajili ya msimu huu ni pamoja na STEVEN BENGO, JOHN NJOROG, JOSEPH SHIKOKOTI ,KABONGO HONORE, JAMAL ROBERT MBA na MOSES ODHIAMBO.

Mwakalebela amesema kamati ya mashindano ya TFF imeipa Yanga kipindi cha siku tano kuweza kuwasilisha jina la mchezaji wanaemkata kwenye orodha yao.

Kabla ya TFF kutoa uamuzi huo tayari timu ya Simba ilishapeleka pingamizi kwa TFF kuhusu Yanga kumuengea Owino kwenye kipindi ambacho sio rasmi.

Wakati huo huo katika hatua nyingine TFF imesema itapeleka tena wakaguzi wake wa viwanja kwenye viwanja vyote zinavyotumika kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu wiki moja kabla ya kuanza michuano hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya TFF ambae pia ni makamu wa pili wa Rais wa TFF Ramadhan Nassib amekili kuwa baadhi ya viwanja havipo kwenye hali nzuri ila anaimani vitakamilika hivi punde kabla ya kuanza kwa ligi hiyo hapo August 23.

Baadhi ya viwanja vyenye matatizo ni pamoja Sokoine Mbeya na Maji maji Songea lakini pia kuna vingine ambazo tayari wahusika wameshapewa maelekezo ya kufanyia kazi.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments