ST George yavunja”Ndoa”yake na Ivo Mapunda

Timu ya ST George ya Ethiopia imesitisha mkataba wake na kipa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Ivo Mapunda aliekuwa akicheza soka la kulipwa kwenye timu hiyo.

Ivo alijiunga na timu hiyo ya ligi kuu nchini humo akitokea timu ya Yanga Africa ya hapa Tanzania mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2008 na kuingia nayo mkataba wa miaka miwili.

Akiongea kwenye kipindi cha michezo cha kila siku cha Radio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inyoitwa TBC Taifa Ivo amesema yeye alirudi nyumbani kwaajili ya mapumziko ila ameshituka kupata habari hizo.

Habari hizo amezipata kwa njia ya Email jioni ya leo jumanne August 11/ 2009 ambayo imetumwa na kocho wa timu hiyo ya ST George Msebia Micho ambae kwa mujibu wa Ivo haina maneno mengi zaidi ya kusema wamestisha mkataba wake.

Akiongea kwenye kipindi hicho cha michezo cha TBC Taifa Ivo amesema kwa sasa atakachofanya yeye ni kufuatilia maslahi yake maana alipojiunga na timu hiyo aliingia nayo mkataba wa miaka miwili na kipindi hicho bado hakijaisha.

Akizungumzia kuhusu kwa sasa ataenda wapi kucheza soka maana hapa Tanzania dirisha la usajili limeshafungwa amesema mameneja wengi wa timu mbalimbali hapa barani Africa wamekuwa wakimsaka na sasa ataanza rasmi kufanya nao mazungumzo.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments