TFF yataka makatibu ndani ya vilabu vya ligi kuu-Mwakalabela

Shirikisho la soka nchini TFF limevitaka vilabu vya soka vya ligi kuu Tanzania bara kuharakisha mchakato wa kupata viongozi watendaji wa vilabu vyao kabla ya msimu wa mpya wa ligi kuu Tanzania bara haujaanza mwezi ujao.

Nafasi ambazo zinatakiwa kuwa na viongozi watendaji  wa kuajiliwa ni pamoja na Katibu mkuu, Msemaji na Mweka Hazina wa klabu.

Katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela amesema hilo ni azimio la mwaka 2007 lililofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani baina ya viongozi wa vilabu hivyo na TFF  ambapo vilabu hivyo vilikubaliana kuwa na viongozi hao, huku azimio la mwaka 2010 likiwa ni la kuboresha miundombinu ya vilabu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanja vya klabu.

TFF imesema hadi sasa hakuna timu hata mmoja ya ligi kuu  iliyopeleka jina la mtendeji wake wa kuajiliwa na TFF inasema bila kufanya timu husika hatoruhusiwa kushiriki ligi kuu msimu ujao.

TFF ilikutana na viongozi wa timu hizo za ligi kuu hapoa jana Jumanne na mkutano huo utaendelea tena hapo kesho Alhamis kujadili mambo mbalimbali yahusuyo msimu mpya wa ligi hiyo

Wakati huohuo, Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetuma barua ya kupendekeza mfumo mpya wa kalenda ya mashindano yake ya  kombe la Shirikisho na lile la  ligi ya Mabingwa barani Afrika, pendekezo ambalo limekubaliwa na TFF.

Katibu huyo wa TFF Mwakalebela amesema TFF imekubaliana na CAF kuhusiana mabadiliko hayo kutokana na kuendana sambamba na kalenda ya TFF inayoanza mwezi July na kukamilika mwezi May kila mwaka husika wa msimu wa soka.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments