Wawili waenda kucheza Canada

Wachezaji wawili wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir  Haroub Canavaro anaechezea mabingwa wa ligi kuu Tnzania bara YANGA na NIZAR KHALFAN pia anaechezea timu ya ligi kuu ya Moro United wameondoka leo Alhamis july pili saa moja asubuhi kwenda nchini Canada kucheza soka la kulipwa kwenye timu ya ligi daraja la kwanza ya VANCOUVER  WHITE CAPS

Akizungumza na tovuti hii  anaeshughulikia swala la uhamisho wa wacheaji hao RAHIM ZAMUNDA KANGEZI amesema wachezaji hao katika safari yao watapitia LONDON – UINGEREZA ili kuweza kupata ushauri wa soka la kimataifa na kesho jioni wataondoka kwenda CANADA

KANGEZI amesema tofauti na hapo awali ambapo walitakiwa kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye timu hiyo ila hivi sasa watasajiliwa moja kwa moja na timu hiyo  kama wakifanikiwa kufuzu vipimo vya Afya zao

Kabla ya kuondoka hapa nchini CANAVARO na NIZAR hapo jana waliongea na kocha wa timu hiyoa ya VANCOUVER  WHITE CAPS pamoja na meneja mkuu wake ambao wamewahaidi kuwajili moja kwa moja baada ya kuvutiwa na vipaji vyao baada ya kuwafanyia utafiki wa kina

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments