Tanzania yapanda katika orodha ya FIFA

Shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka ulimwenguni ambapo TANZANIA ipo katika nafasi ya 97 kwa ubora wa soka ulimwenguni.

Viwango hivyo ni vya mwezi JUNE hadi JULAI ambapo TANZANIA awali ilikuwa katika nafasi ya 109 ulimwenguni.

national-flag

Wakati huohuo IVORY COAST imeipiku CAMEROUN kwa kuwa timu ya kwanza Afrika kwa ubora wa viwango vya soka barani Africa

Afisa habari wa TFF – Floriani Kaijage amesema Ubora wa viwango hivyo umepanda unatokana na michezo ya kirafiki iliyocheza timu ya taifa (Taifa Stars) mbapo ilicheza na NEW ZEALAND na kuifunga magoli MAWILI kwa MOJA.

Mchezo huo ulichezwa June tatu kwenye dimba la Taifa na Taifa Stars ilipata ushindi huo kwa magoli ya Jery Tegete na Mwinyi Kazimoto

Akizungumzia kupanda kwa Tanzania kwa ubora wa soka Duniani kwa  nafasi 12 kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo amesema ni hatua nzuri kwa soka la Tanzania

Maximo anasema si Kazi ndogo hata kidogo kufikia nafasi za chini ya mia moja ila sio kulilia kupanda katika ubora wa FIFA pia inahitajika kuimalisha soka letu

Kocha huyo amesema kitu kingine kitakachosaidia kukuza soka la Tanzania ni kwa wachezaji wake wengi kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi maana wakirudi watalisaidia taifa na kuleta changamoto kwa wenzao

Pia amepongeza wachezaji watatu wa timu ya taifa kwenda kujaribu bahati ya kucheza soka la kulipwa njee ya nchi, wachezaji hao ni Henry Josep alieenda nchini Norway, Nadir Haroub (Canavaro) na Nizar Khalfan wanaotarajiwa kwenda Canada kufanya majaribio ya kucheza la kulipwa

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments