TBF kufanya kozi Tanzania

Tunategemea kufanya basketball coaching course na mkufunzi toka Nairobi, kozi hii inatambuliwa na FIBA Africa. Itafanyika June 23-29, 2009.

Makocha wote wanaotaka  kufanya kozi hii ambayo itajkua pia na mtihani na watakaopasi watatambuliwa na FIBA Africa wajiandikishe mapema maana nafasi ni chache na makocha wote watajigharamia kila kitu.

July 27 – 2August

Klabu bingwa Zone 5 itafanyika Kampala Uganda na timu za Jeshi (ABC na JKT) zimethibitisha kushiriki mashindano haya, nchi zingine katika ukanda huu ni Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Somalia.

August

Ligi ya Muungano inategemewa kufanyika Dsm, TBf inasubiri majina ya timu nne za wanawake na wanaume toka zanzibar. Timu za bara zitazowakilisha mashindano haya ni ABC, JKT, Mzinga na Dodoma spurs na kwa wanawake ni Jeshi stars, JKT queens na Cargo ladies.

October

Taifa cup na uchaguzi mkuu wa TBF, bado hatujateua mkoa wa kufanyikia mashindano hayo

Tunategemea kuwa pia na clinic ya vijana chini ya miaka 16 itakayofanyikia pia Dsm kwenye uwanja wa International school masaki kati ya tarehe 19-23 October na mkufunzi toka spain

lawrence Cheyo

Katibu mkuu TBF

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments