Kuweni na Gym zenu-Maximo

KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amevishauri klabu zinazoshiriki ligi kuu kuwa na vituo vya mazoezi ya vingo (gym) ili kupata wachezaji wazuri wa timu hiyo.

Maximo alisema ni muhimu kwa klabu zote kuwa na utaratibu wa kuwa na gym kwa ajili ya wachezaji wao kuwa kuwa fiti kiafya na nguvu.

Alisema hivi karibuni gym kwa ajili ya timu ya Stars itakuwa tayari kwa ajili ya wachezaji hao kufanya mazoezi ambayo watafanya kwa wiki mara tatu ili kujiweka safi.

Alisema faida ya kwa mchezaji kufanya mazoezi gym ni kumsaidia kwa vitu vingi katika mpira na ndio maana kunakuwa na siku ya kufanya mazoezi hayo gym na kufanya kupata wachezaji wenye nguvu na uwezo mkubwa katika soka.

Alisema kuwa gym hiyo itakuwa kwa wachezaji wa timu ya taifa tu na hata timu hiyo isipokuwa kambini kutakuwa kutakuwa na siku maalum kwa wachezaji hao kwenda kufanya mazoezi katika siku zitakazopangwa.

Kocha huyo aliwapongeza mashabiki wote kwa uzalendo walioonyesha siku ya mechi dhidi ya New Zealand na Stars na kuwataka waendelee na moyo huo huo kwani hali hiyo itawafanya wazidi kufanya vizuri katika mechi zao nyingi.

Alisema kuwa ushindi huo wa Stars walikuwa wameuandaa tangu siku 15 zilizopita na walitegemea kushinda na alifurahia chipukizi wake ambao walionyesha kiwango cha juu katika mechi hiyo.

Wakati huo huo, Kampuni ya Samsung Tanzania jana ilikabidhi televisheni na deki vyenye thamani ya Shilingi milioni moja kwa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF).

Afisa Masoko wa Samsung, David Joseph alisema kuwa wametoa msaada huo kwa TFF, ili kuweza kuwarahisishia kazi na kuendesha mambo yao kisasa zaidi.

Alisema msaada huo hautaishia katika zawadi hizo na kwamba wataendelea kuisaidia TFF, ili kuendesha mpira kisasa zaidi na kuyataka makampuni mengine kufanya hivyo ilikukuza mchezo huo nchini.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments