TFF yavionya vilabu juu ya Taifa Cup

Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) limepinga vikali hatua iliyochukuliwa na baadhi ya timu za ligi kuu Tanzania bara kuwazuia wachezaji wao kutocheza michuano ya kombe la Taifa

Hatua hiyo imekuja baada ya mwenyekiti wa timu ya Simba Hassan Dalali hapo kutoa taarifa ya kuwazuia wachezaji wa timu hiyo kuitwa kwenye timu mbalimbali za mikoa inayoshiriki michuano ya kombe la Taifa ya mwaka huu

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Sunday Kayuni amesema wao wanachojua msimu wa soka kwa wao TFF unaisha mwishoni mwa mwezi huu na hakuna timu yenye amri ya kuzuia wachezaji wake wasishiriki michuano ya kombe la Taifa

Kayuni amesema kama kuna mchezaji atakaeitwa na timu yeyote ile ya mkoa kwaajili ya michuano hiyo ya kombe la Taifa na asiende basi atachukuliwa hatua kali za kisheria

Wakati huo huo TFF imesema vitendo vya wachezaji kutaka pesa nyingi ilikuchezea mkoa unaomtaka kwenye michuano hiyo ya kombe la Taifa ni kinyume cha sheria na wao wanasema kama wakipata taarifa hizo basi watamchukulia hatua kali za kisheria mchezaji husika maana kuitwa kwenye timu ya mkoa hakuitaji pesa

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo wa ufundi wa TFF anasema mikoa yenye timu za ligi kuu zinapewa nafasi kubwa ya kuwatumia wachezaji kwenye taifa Cup pia anazuia kuitwa kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuitwa kwenye timu za mikoa mbalimbali kwa michuano hiyo ya kombe la Taifa

Taifa Stars hivi sasa ipo kambini ikijianda na michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Congo DRC ambayo ni bingwa wa Africa kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya nchi inayotua leo hapa nchini tayari kwa mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments