DRC kutua Dar Leo

Timu ya taifa ya Kongo (DRC) inatarajiwa kuwasili leo Jumatano katika makundi mawili tofauti tofauti tayari kwa mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) utakaochezwa jumamos ijayo kwenye dimba la Taifa hapa jijini Dar es salaam

Kundi la kwanza la watu 14 watakaotokea Kinshasa linatarajia kuwasili Dar es Salaam saa 12.35 jioni wakati kundi la pili la watu 11 litakalotokea mjini Lubumbashi litawasili saa 3.10 usiku.

kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa habari wa TFF Florian Kaijage inasema kundi linalotoka Kinshasa linajumuisha viongozi wa ufundi na wachezaji wanaotoka katika vilabu mbalimbali isipokuwa wachezaji toka klabu moja ya TP Mazembe yenye makao yake mjini Lumbumbashi ambayo wachezaji wake na baadhi ya viongozi ndiyo watasafiri kutokea katika mjini huo.

Timu ya DRC inayokuja inajumuisha wachezaji wote nyota wa kikosi kilichotwaa ubingwa wa michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani iliyofanyika huko Ivory Cost mapema mwaka huu.

Kaijage anasema wachezaji hao nyota ni pamoja na mchezji bora wa fainali hizo MABI MPUTU na mlinda mlango MUTEBA KIDIABA

DRC LIST OF DELEGATION

KINSHASA – DAR – KINSHASA

BINAMUNGU THEO

MUNTUBILE SANTOS

LOKOSE EPANGALA

KABASU BABO

MBUNGU KAKALA DR.

KIMUAKI JOEL

BOKESE GRADYS

SALAKIAKU MATONDO

LOFO BONGELI

NDAYA MBANGI

EBUNGA SIMBI

MAKIESE KIENTURI

DIBA ILUNGA

ERIC BOKANGA

LUBUMBASHI – DAR – LUBUMBASHI

NKULU KABWE

MAYAMONA NDONGALA

KIDIABA MUTEBA

MABELE BAWAKA

KASONGO NGANDU

MIHAYO KAZEMBE

KALUYITUKA DIOKO

BEDI MBENZA

MPUTU MABI

TSHANI MUKINAYI

NKULUKUTA MIALA

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments