TFF, Yawathibitisha makocha wa U17,U20 na viungo

Shirikisho la soka nchini TFF limewatangaza makocha wasaidizi wawili wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambao ni Rodrigo Stokler ambae pia ni kocha wa timu za taifa za vijana za chini ya miaka 17 na 20.

Na mwingine ni kocha wa viungo anaeitwa Marcelo Guerreiro wote ni toka nchini Brazil watakaoshirikiana na kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars,Marcio Maximo.

Akiwatangaza mbele ya waandishi wa habari jijini DSM katibu mkuu wa TFF, Fedrick Mwakalabera amesema makocha hao wamefanikiwa kuchaguliwa na kamati ya ufundi ya TFF baada ya kuridhishwa na vigezo vyao

Mara baada ya kutambulishwa kocha msaidizi Rodrigo Stokler ambaye amewahi kufundisha timu ya vijana za Flamingo,Coritiba,Borta fogo za nchini Brazil na timu ya vijana ya Zico Club iliyopo nchini CHINA amesema amefurahishwa na kocha Maximo kwa kumpendekeza kuja kufundisha timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 na 20 za Tanzania

Kwa upande wake kocha wa viungo Marcelo Guerreiro amesema amewaona wachezaji wa Tanzania wakiwa na uwezo mzuri lakini wanakosa nguvu nay eye amekuja kwakazi hiyo ya kuwaongezea nguvu na anahakika atafanikiwa katika hilo

Makocha hao wanachukua nafasi iliyo awachwa wazi na kocha wa timu za vijana za chini ya miaka 20 na 17 Marcus Tinoco ambaye anafundisha nchini Trinad and Tobego na Itamar Amorin aliekuwa kocha wa viungo ambae kwa sasa anafundisha timu ya ligi kuu Tanzania bara ya Azam FC ya hapa jijini DSM.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments