Ligi kuu bara kufikia kileleni kesho

Ligi kuu Tanzania bara inamalizika kesho huku tayari timu ya Yanga ikiwa imeshatawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo kwa kujikusanyia ponti 51 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote ile hadi sasa

Yanga inapointi 51 katika michezo yake 21 iliyocheza huku ikifutiwa na wapinzani wao wa jadi timu ya Simba yenye pointi 37 ambayo yenyewe hapo kesho itacheza na timu ya Polisi Dodoma iliyokwisha shuka daraja.

nadir_haroub

Vita kubwa ya hapo kesho ni kwenye michezo michezo mitatu wa kwanza ni baina ya Simba na Polisi Dodoma ambapo Mnyama Simba analazika kushinda mchezo huo ilikujihakikishia kushika nafasi ya pili ili kuweza kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Africa hapo mwakani 2010.

Vita ya pili itakuwa mjini Morogoro pale timu ya Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya tatu itakaposhuka dimbani kukipiga na timu ya Polisi Morogoro,mchezo huo ni muhimu mno kwa timu zote mbili maana Mtibwa yenye pointi 35 inataka kushinda mcheoz huo huku ikiomba Mungu Simba ifungwe na Polisi Dodoma ili wao washike nafasi ya pili na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa hapo mwakani 2010 hjuku yenyewe Polisi Morogoro yenye pointi 25 inataka kushinda mchezo huo ilikuweza kujihakikishia kubakia kwenye ligi hiyo msimu ujao wa 2009 – 2010.

huko jijini Mbeya nyanda za juu kusini timu ya Tanzania Prisons inayoshika nafasi ya tano kwenye ligi hiyo itacheza na timu ya Moro United yenye pointi 22 inayopigana kutoshuka daraja, timu hiyo ya Moro United  inashuka dimbani huku ikiomba ishinde mchezo huo dhidi ya Tanzania Prisons na pia inaomba Mungu timu za Toto Africa ya jijini Mwanza na Polisi Morogoro zipoteze michezo yapo kitu ambacho ni kigumu kidogo katika soka la Tanzania maana zote mbili zinacheza nyumba huku Moro United wao wakiwa ugenini

hadi sasa tayari timu mbili zimeshashuka daraja nazo ni Polisi Dodoma na Villa Squad ya Dar es salaam ambazo zote zinapointi 15.

wakati ligi hiyo ikimalizika tayari timu tatu zitakazishirikia ligi kuu Tanzania bara msimu ujao toka ligi daraja la kwanza

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments