Maximo awatangazia vita wachezaji wasiojituma Taifa Stars

KOCHA wa Taifa Stars ametoa kauli ya tahadhari kwa wachezaji wote ambao hawana msaada kwenye kikosi chake, wasiotaka ushirikiano na kujituma uwanjani atawaengua kwenye timu hiyo baada ya mashindano.

Maximo alitoa kauli muda mfupi baada Stars kupambana hadi dakika ya mwisho na kuwashinda wenyeji Ivory Coast huku wachezaji kadhaa nyota wa kikosi hicho, Haruna Moshi ‘Boban’ na Athuman Idd ëChujií wakiwa jukwaani bila ya maelezo.

nadir_haroub

Akizungumza katika hoteli ya Golf jijini hapa, Maximo alisema atachukua uamuzi mkubwa wa kufanya mabadiliko katika kikosi chake baada ya mashindano haya na wachezaji watakaopata nafasi ni vijana na Watanzania wasahau tena zile tabia za majina kwa kuwa si yanayocheza.

ìUmeona timu ya leo, wachezaji wameonyesha kutekeleza majukumu yao na upendo kwa taifa. Wamecheza kwa kujitolea, wamejituma kwa nguvu na kwa kuwa nyumbani wameshuhudia mchezo huo watakuwa wameona hilo.

Watu wa namna hiyo ndio wenye nafasi kwenye timu yangu.

ìHakuna nafasi ya majina, hakuna mchezaji nyota kwenye kikosi changu ambaye hana msaada basi tu anachaguliwa kwa kuwa jina lake linajulikana. Kwenye kikosi hiki hakuna, safari ijayo nafasi kubwa ni kwa vijana na si vijana wa umri tu, nataka wawe na mawazo na malengo mapya pia kwa ajili ya faida ya Tanzania,î alisema Maximo.

ìUnajua kuna lawama nyingi ambazo kama utazisikiliza hauwezi kufanya kazi, unajua kama ilivyo ada ya wengi kama timu ikifanya vizuri sifa zinaenda kwa wengine na ikifanya vibaya basi ni lawama za kocha. Bora iwe hivyo lakini nataka timu ifanye vizuri.

ìHuu ni wakati mwafaka wa kujenga kikosi kipya cha Tanzania chenye wachezaji wenye nidhamu na uwezo wa kujitolea kwa ajili ya taifa lao. Na si wenye majina makubwa yanayojulikana kwa watu wa taifa lao, lakini hawana msaada wowote kwa watu wa taifa lao,î alisisitiza.

Alipoulizwa sababu ya kutowachezaji Haruna Moshi na Athuman Idd walikuwa katika kiwango kizuri, Maximo alijibu kwa ufupi tu. ìHii ni timu, si mtu mmoja mmoja na tunaangalia nani yuko tayari kwa ajili ya mechi.î

Akizungumzia mchezo huo dhidi ya Ivory Coast, Maximo aliwapongeza wachezaji wake kwamba walicheza kwa kujitolea. ìMsimlaumu mtu, mfano Henry aliumia muda mrefu.

Alitaka kutoka nikamwambia ajitahidi hata dakika 20 kwanza. Alifanya hivyo akiwa na maumivu lakini lengo lilikuwa ni kulisaidia taifa lake. Angalia wengine kama Kingi, kacheza kwa nguvu zote. Nawapongeza sana.î

Stars inahitaji kushinda mechi ya kesho dhidi ya Zambia kwa idaidi yoyote ili ipate nafasi ya kusonga hadi hatua ya nusu fainali huku Chipolopolo ikiwa inahitaji sare tu kupata nafasi ya kusonga mbele.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments