Tenisi sasa yapelekwa mashuleni

CHAMA cha Tenisi Tanzania(TTA) wapo mbioni kuanzisha mpango maalumu wa kufundisha mchezo huo katika ngazi za shule za msingi na sekondari kwenye mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro, Arusha, Dodoma, Mwanza na Kilimanjaro itahusika katika awamu ya kwanza.

Mpango huo uliopitishwa hivi karibuni katika mkutano wa wadau wa chama hicho uliokuwa unajadili mipango ya maendeleo ya mchezo huo kwa mwaka 2009.

Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa TTA Denis Makoi alisema kuwa mpango huo utagharimiwa na chama chake kwa kushirikiana na Shirikisho la Tenisi la Kimataifa(ITF).

Alisema kuwa katika kufanikisha hilo chama chake kitatoa walimu watakaokwenda mikoani kwaajili ya kutoa mafunzo hayo na kuongeza kuwa kwa mwanafunzi atakayekuwa tayari atatakiwa kulipa kiasi kidogo cha fedha .

Makoi alisema kuwa kwa kuanzia mpango huo utaelekezwa kwa baadhi ya shule zilizoko jirani na Klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam.

“Lengo ni kuueneza mchezo huu nchi nzima na katika kufanikisha hilo tutaanza na mikoa mitano kwanza ambapo tutatoa mafunzo kwenye shule za msingi na sekondari”alisema Makoi.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments