BMT waipongeza TFF

BARAZA la Michezo la Taifa, BMT, limelipongeza Shirikisho la Soka Tanzania TFF kwa kuwa na mipango madhubuti iliyoiwezesha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kufanikiwa kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani, CHAN.

leodgar-tenga

Akifafanua tathimini ya maendeleo ya michezo yote kwa ujumla kwa mwaka uliopita, Mwanyekiti wa BMT, Iddi Kipingu alisema kwa kiasi kikubwa kati ya michezo iliyoweza kufanya vizuri katika mwaka uliomalizika ni soka kwani kwa kiasi kikubwa umeonyesha ukomavu.

Taifa Stars ilifanikiwa kufuzu fainali hizo baada ya kuichapa Sudan mabao 5-2.

Alisema TFF kwa kusaidiana na makampuni pamoja na wizara husika wamesaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha timu ya kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo ambapo kwa mara ya mwisho ilikua ni miaka ya themanini.

“Soka kwa mwaka jana ilitupa hamasa sana mashabiki na sisi kama BMT hatuna budi kutoa tathmini yetu kwa kazi nzuri waliyoifanya hasa kwa kocha wao Maximo ambaye ameonyesha utaalamu wa hali ya juu hadi kufikisha timu hadi mahali ilipo ya kuweza kushiriki fainali kama hizi,” alisema Kipingu.

Alisema uzoefu na ukomavu wa wachezaji katika mashindano mbalimbali utawapa changamoto zaidi hivyo kuweza kushiriki kombe la dunia.

Aidha alilitaka shirikisho hilo kuzingatia ligi za watoto ziboreshwe zaidi pamoja na kuendeleza michezo mashuleni kwa ajili ya kupata vipaji vipya kwa maendeleo ya mchgezo wa soka zaidi.

Kipingu pia alisifia uchaguzi uliomalizika wa viongozi wa shirikisho hilo kutokana na kuwa wa kidemokrasia zaidi na kuwataka viongozi wapya kubuni mikakati na malengo mapya kwa ajili ya kuinua zaidi mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments