Tanzania yapoteza kwenye tenisi

Timu ya Tanzania imeshindwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya tenisi kwa wachezaji wawili wawili baada ya wachezaji wake kupoteza michezo hiyo ya kufuzu kwa robo fainali.

Wachezaji wenye umri wa miaka 14, Nikita Daula na Michele Onyancha wa Kenya waliwatambia Zuhura Baraka na Melesa Brown wa Tanzania kwa kuwafunga kwa seti 2.0 matokeo yakiwa 6-0,6-0 na huku chipukizi wa Ethiopia, Semira Micheal na Samerawiti Teklu wakiibuka kifua mbele kwa kuwafunga Lyola Lukas na Shivan Sursak wa Tanzania kwa seti 2.0 ikiwa 6-0,6-0

Katika michezo mingine Ndayisenga Idrisa na Ndayishimiye Hasan wa Burundi waliwafunga Oringa David na Ayella Simon wa Uganda kwa 6-0,6-1.

Siku hiyo iliendelea kuwa mbaya kwa Watanzania kwa kushudia Fabian Festo na Loti Hema wakifungwa na wachezaji wa Kenya, Gibraela Teja na Derick Onyancha kwa 7-6,6-3 na Warundi Irankunda Santaina na Syori Laula waliendeleza dozi dhidi ya Hadija Swalehe Zkir Salum kutoka Tanzania

Wachezaji Shufaa Changawa na Nadia Fernandes wa Kenya waliwabwaga wenyeji Tanzania, Violet Peter na Zuhura Salum kwa seti 2.0 matokeo yakiwa 6-1,6-3 na Waburundi Iradukund Guy na Ntatangwa Robin waliwafunga Shaabaan Ibrahim na Hafidh Hamis wa Tanzania kwa 6-1,6-2, wenye walipata ushindi pekee kutoka Ismael Changawa na Shaaban Ibrahim wao waliibuka na ushindi wa seti 2,0 ikiwa 6-0,6-0

Wachezaji wa Tanzania waliofanikiwa kutinga robo fainali ni Shaaban Yasin ataonyeshana kazi na Teame Gabresalasie wa Ethiopia, wakati Violet Peter akicheza na Fermandez Nodia wa Kenya na huku Irankunda Santiana wa Burundi akicheza na Mtanzania Salehe Hadija naye Zakia Salum akicheza na Shufaa Changawa na Justin Joseph wa Tanzania akicheza na Hema Loti

Mchezaji Teja Gibrael wa Kenya atapambana na mchezaji kutoka Burundi Ndayisenga Idrisa naye Mtanzania mwingine alitinga robo fainali Hafidh Hamis atacheza na Gatete Hamis kutoka Rwanda huku Mtanzania Shaaban Ibrahim atacheza na Mtanzania mwenzake Tumain Martin na Gregory Iradukwinda wa Burundi atacheza na Mateois Amsaku wa Ethiopia.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments