Ziara ya Real Madrid Tanzania yaibuka upya Bungeni

UJIO wa timu ya Real Madrid ya Hispania, umeibuka tena bungeni baada ya kambi ya upinzani kuibua tena suala hilo na kutaka serikali itoe tamko kama timu hiyo itakuja au la.

Katika hotuba mbadala ya Wizara ya Habari, Utamduni na Michezo iliyotolewa na waziri kivuli jana Mwanawetu Said Zarafi, kambi hiyo ilisema ujio wa timu hiyo ulielezwa ni moja ya mafanikio ya ziara za Rais Jakaya Kikwete, nje ya nchi.

Alisema serikali iliwahi kutoa tamko la ujio wa timu hiyo na kufanya michezo ya kirafiki Julai mwaka jana na kuhoji, ”kambi ya upinzani inauliza ujio wa timu hii ni lini?”

”Je, Rais alipotoshwa, kuna jambo gani hapo, kama imeshindikana ni kwanini serikali inakosa ujasiri wa kalieleza Taifa kilichojiri kama ilivyotamkwa rasmi na kwa mbwembwe wakati wa kutangaza uwepo wa utaratibu huo?”

Kambi hiyo ilisema, kwa kuzingatia ukweli huo inataka kupata uhakika kama kweli timu itakuja na ni lini hasa.

Msemaji huyo aliongeza kwamba, kambi hiyo pia inataka wizara itoe takwimu ni kiasi gani cha fedha ambacho kitatumika iwapo timu hiyo itakuja nchini.

”Sambamba na hilo, inataka kufahamu mpaka sasa serikali imetumia kiasi gani cha fedha kwenye maandalizi ya ujio wa timu hiyo, hasa ukizingatia kuwa kamati ilikwishaundwa na shughuli za uandajaaji na kazi zilikwishaanza kama ilivyotangazwa ndani ya bunge lako tukufu.”

Ujio wa Real Madrid umebaki kuwa ndoto kutokana hadi sasa kutofahamika hasa, nini

kilisibu mpango huo kuzimika ghafla kama mshumaa.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments