TFF, CECAFA walituhadaa – Madega

Uongozi wa Yanga, umelitupia lawama Shirikisho la soka nchini (TFF) na Baraza la soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuwa uliwahadaa kwenye suala la mgao wa mapato ya mchezo wao kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Simba, uliokuwa umepangwa kuchezwa kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, jijini, Dar es Salaam, ambapo Yanga haikujitokeza uwanjani.


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Imani Madega alisema kuwa awali walikubaliana kuingiza timu uwanjani mara baada ya wao pamoja na watani zao wa jadi Simba kupewa fedha ambazo waliafikiana.

Alisema muda mfupi kabla ya muda wa mchezo kufika walikaa viongozi wa timu zote mbili pamoja na viongozi wa TFF na CECAFA, ambaopo walikubaliana masuala mbalimbali kabla ya mchezo kitu ambacho kilikubaliwa na pande zote na kuafikiana kuwa utekelezaji utafanyika kabla ya mchezo.

Madega, alisema kuwa cha kushangaza hakuna kilichotekelezwa na badala yake wakashangazwa na hatua ya watani zao Simba kutinga uwanjani jambo ambalo liliwafanya wao kukataa kupeleka timu kwa madai kuwa kuna mbinu zitakuwa zimefanyika ili kutotekeleza makubaliano.

“Tulikubaliana pande zote kuwa tutapeleka timu mara baada ya kutekelezewa matakwa yetu, lakini nimeshangaa kuona wenzetu wamebadilika, tunajua kulikuwa na namna ambayo ingetumaliza,“alisema Madega.

Madega aliongeza kuwa kilichowafanya Simba wakiuke makubaliano ni njaa ambayo
inaweza kuwapeleka pabaya kama hawatakuwa na msimamo katika maamuzi yao.

Alisema wanajua wazi kuwa michuano hiyo ilikuwa ikiendeshwa na timu za Simba na Yanga,ambapo walichokitaka wao ni kuhakikisha kuwa timu hizo zinafaidika na si kuwanufaisha watu wengine.

Aliongeza kuwa uongozi wake utaendelea kuwa na msimamo thabiti, ambapo hawatahofia chochote kitakachojitokeza mbele ya Wakati huo huo, uongozi wa Yanga ulitarajiwa kukutana jana ili kujadili adhabu ya kufungiwa miaka mitatu waliyopewa na CECAFA.

Madega aliahidi baada ya kikao hicho kuwa angelipua bomu kuhusu uendeshaji wa mashindano hayo.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments