TFF yatoa somo kwa ZFA kuhusu mgawo toka Fifa

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limewataka wenzao wa Zanzibar, ZFA kuacha kung’ang’ania mgao wa fedha zinazotoka Shirikisho la Kimataifa (Fifa) likisema mgao huo huja na masharti ambao visiwa hivyo hufaidika.

Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema jana kuwa katika kikao cha kesho, TFF itawapa ZFA nyaraka zinazoonyesha masharti ya fedha hizo za Fifa ili kuondoa lawama.

”Fedha zao huja zikiwa wamezipangia kazi, “alisema Mwakalebela. ”Kunakuwa na kozi za utawala, ufundi, uamuzi, tiba ya michezo, miundo mbinu, soka la wanawake, na vyote hivvo Zanzibar wamekuwa wakifaidika navyo. Tutawapa makabrasha yote ya Fifa Development.”

Mpango huo wa maendeleo wa Fifa ni kwa nchi zianzoendele na kwa upande wa kusini mwa Afrika husimamiwa na Ashford Mamelody.

”Tuna mkataba wa miaka 10 na Fifa na kila mwaka hutoa dola 25,000. Tulipoweka kambi ya timu ya taifa ya wanawake ilitugaramimu Sh 120m ambayo ni mara sita ya fedha za Fifa. Halafu kiasi hicho tena tugawane sasa hapo tutagawana za nini?

”Tunawashauri ZFA wabuni miradi ambayo itawaingizia kipato badala ya kushikia bango fedha za Fifa ambazo zimejaa masharti kibao.”

Wakati huohuo Mwakalebela amepinga madai yaliyotolewa na makamu mwenyekiti wa ZFA, Haji Amir kuwa mechi ya Miembeni na Yanga iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Yanga kutoka kifua mbele kwa bao 1-0, ilihujumiwa.

”ZFA na Miembeni wasitafute sababu za kujilinda zisizo na msingi,” alisema. ”Baada ya kufungwa, kocha ambaye ndio mwenye taaluma alikiri kwua kiwango kipo chini, mfumo wa ligi ya ZFA unaua soka badala ya kujenga.

”Mechi ya kwanza walishinda kwa bahati. Warekebishe mfumo wa ligi yao ili iwe bora. Tutawapa mwongozo kama watautaka ili wawe na ligi bora kama ya kwetu.�

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments