TFF kuukarabati uwanja wa nyamagana

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga ameieleza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwa iwapo Uwanja wa Nyamagana hautabadilishwa matumizi, shirikisho lake litauchukua na kuutunza.

Tenga aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa shirikisho lake limesikitishwa na taarifa za kutaka kubadilisha matumizi ya uwanja huo wakati jiji wa Mwanza bado likiwa linahitaji viwanja nane kwa ajili soka.

Alisema iwapo uwanja huo utabakia na kukabidhiwa mikononi mwake chini ya chama cha soka mkoa, uwanja huo wataukarabati ikiwa ni pamoja na kuuwekea nyasi bandia ili uwe ukitumuka katika michuano mbalimbali ikiwemo ya watoto wa sekondari na ligi ngazi za mkoa.

Kulingana na ukubwa wa jiji la Mwanza viwanja vya mipira ambavyo vinapaswa kuwepo ni zaidi nane na kufafanua kuwa kuwa kuwepo kwa Uwanja wa CCM Kirumba ambao una uwezo wa kukaliwa na watazamaji 25,000 hautoshi, alisema.

Akieleza kuhusiana na Nyamagana, Tenga aliwaasa wale wanaotoa hoja kuwa uwanja huo ni mdogo wanapaswa kuitambua kuwa katika mchezo wa soka kuna viwanja vya aina mbili na kutoa mfano wa Uwanja wa Emirates wa klabu ya soka ya Arsenal kuwa ndio uwanja pekee wa mpira wa miguu.

Katika soka kwa sasa kuna viwanja vya soka aina mbili, kuna uwanja ambao unakuwa ukijumuisha sehemu ya michezo mingine kama riadha lakini viwanja vya sasa ambavyo ni maalumu kwa ajili ya soka vinakuwa na sehemu ya kuchezea na sehemu za kukaa mashabiki, alieleza.

Alisema katika aina hiyo ya pili ya uwanja mashabiki kwa sasa wamekuwa wakikaa karibu kabisa na uwanja kiasi cha umbali wa mita tano hii ni kutokana na kutaka kuwasogeza mashabiki karibu na wachezaji ili kuongeza mzuka wa soka.

Tenga alisema kama suala ni biashara bado anaamini kuwa uwanja wa soka unawezwa kuwepo na soka likaendela kuchezwa huku uwanja huo ukiwa umezungukwa na maduka na kutoa mfano wa uwanja Zamelek ambao licha ya kutumika kwa soka pia umezungukwa na maduka.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments