Kiingilio cha kuwaona stars Mwanza ni mzigo kwa wananchi!

KIINGILIO cha mechi ya timu ya Tanzania,Taifa Stars na Uganda, The Cranes, itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kimelalamikiwa na mashabiki wa soka hapa kuwa ni kikubwa.

Shirikisho la soka Tanzania, TFF limetangaza kuwa watakaotaka kuuona mchezo huo watalazimika kulipa sh,5,000 kwa mzunguko na sh,20,000 kwa jukwaa kuu.

Nizar Khalfan

Baadhi ya mashabiki wameanza kugwaya na kupanga kuusikiliza mchezo huo kupitia redio na kwa kile walichodai kuwa kiingilio ni kikubwa.

Taarifa mbalimbali zilizokuwa zikipatikana jijini humo kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa soka tangu kutangazwa kwa kiingilio hicho zilikuwa zinasema kwamba kiingilio hicho ni kikubwa mno kiasi kwamba mashabiki wengi hawataweza kumudu hali ambayo inaweza kupunguza mapato kwa timu hizo.

Msemaji wa TFF nchini Florian Kaijage aliviomba vyombo vya habari jana jijini hapa kuwaelimisha wapenzi wa soka kuwa hicho ni kiingilio cha kawaida kutokana na gharamaza uendeshaji wa mechi hiyo.

Kaijage alisema kuwa kiingilio hicho sio mara ya kwanza kutumika kwa mechi kubwa katika jiji la Mwanza ispokuwa vyombo vya habari vinatakiwa kusidia TFF kuwaelimisha wapenzi ili wajitokeze kwa wingi.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments