Timu ya Zanzibar U20 Kwenda Misri kwa mazoezi

TIMU ya taifa ya Vijana Zanzibar chini ya miaka 20, Karume Boys inatarajiwa kuondoka nchini kesho kuelekea Cairo Misri ambako itacheza mechi za kirafiki za kujiandaa na michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati.

Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Agosti jijini Nairobi, Kenya yatashirikisha timu za Tanzania Bara na Visiwani .

Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Massoud Atai Masoud alisema jana kuwa maandalizi ya safari hiyo yameshakamilika na kwamba kikosi hicho kitakuwa kambini chini Misri chini ya kocha Badri El-din Hadad, kutoka Misri na msaidizi wake, Masoud, ambaye ni Mzanzibari.

Kikosi hicho kinaundwa na Abdulkhan Gulam Abdallah, Amour Suleman Kombo, Mohammed Juma Azam, Abass Seif Ali na Haji Abdi Hassan na Omar Juma Ali (Malindi), Hassan Rashid Nasid

Wengine ni Saleh Juma ( Small Simba) Ishak Othman Omar, Salum Said Salum, Mohammed

Abdul Shaali ( JKU), Mohammed Abdalla Khamis, Ali Hamza Omar ( Mlandege) Said Khamis

Abdalla, Mzee Ramadhani (Duma) na, Nassor Ali Omar kutoka Sharp Boys ya Nungwi.

Wamo pia, Hamid Ali Rajabu, Suleiman Kassim Suleiman, Haji Ramadhani Mwambe na Abdi

Nassor Mohammed (Mafunzo), Nahoda Bakar Haji wa Polisi na Idrissa Abdulrahim Shaaban kutoka kikosi cha KMKM.

Kikosi hicho kitarudi nchini Mei 25 na kumalizia mafunzo kwa kucheza na klabu zitakazoshiriki michuano ya Afrika Mashariki ya Kati kwa lengo la kujipa makali zaidi.

Ziara hiyo ni ya pili kwa vijana hao walio chini ya umri wa miaka 20 kwenda Misri kwa ajili ya kujitayarisha na kupata mazoezi zaidi nchini humo.

Comments