Bendera aongoza mazishi ya aliyekuwa katibu mkuu wa BFT

Naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo, Joel Bendera jana ameongoza mazishi ya aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la ngumi Tanzania- BFT, Gaston Mlay.

Akitoa salam zake wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika katika makaburi ya kinondoni jijini Dar es salaam, naibu waziri amesema marehemu Mlay atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza mchezo wa ngumi nchini.

Katika tukio jingine naibu waziri amepokea hundi kutoka kampuni ya bia ya Serengeti yenye thamani ya shilingi milioni tatu, laki saba na 50-elfu, pamoja na tiketi mbili za ndege kwa ajili ya mabondia sita wanaoondoka nchini jumamosi hii kuelekea namibia kwa michuano ya kufuzu kushiriki mashindano ya Olimpik yatakayofanyika nchini China mwaka huu.

  • SOURCE: ITV

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments