Mchezaji Judo Masoud Amour wa Zanzibar amechaguliwa kuwa mwanamichezo bora

Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania- TASWA, kimemchagua mchezaji Judo Masoud Amour wa Zanzibar kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Februari mwaka huu.

judo-picture.jpg

Uchaguzi wa mwanamichezo huo umefanyika jijini Dar es Salaam ambapo katibu msaidizi wa TASWA, Amir Mhando amesema Masoud ametwaa nafasi hiyo baada ya kupata alama 101 na kuwashinda wenzake Faraja Malaki aliyepata alama 76 na Semeni Mlanzi aliyepata alama 75.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments