4,000 wachuana Kilimanjaro Marathoni

Tanzaniasports::Where Sports People Meet


 

Zaidi ya wanariadha 4,000 wanatarajia kutoana jasho katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni yatakayofanyika leo mjini hapa.

08-hk.jpg

Kwa mujibu wa waandaaji Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika ndiye anayetarajia kuwa mgeni rasmi katika mbio zitakazoshirikisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi, akiwemo mshindi wa mwaka jana Andrew Cyliv aliyetumia saa 2:18.47.

Hata hivyo, muda wa wastani wa kumaliza mbio za kimataifa za marathon zenye hadhi zaidi ni saa 2:08.

Kwa mujibu wa daftari la usajili, mshindi wa tatu wa mbio za nyika za Afrika Mashariki zilizofanyika mjini hapa wiki iliyopita Jumanne Tulway naye amejiandikisha kwa mashindano hayo.

Mbali na mbio za marathon, pia kutakuwa na mbio za nusu marathon ambazo miongoni mwa watakaoshiriki ni Martine Sulle.

 

Mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 42 (marathoni) atazawadiwa shilingi milioni 3 kwa wanawake na wanaume.

Mashindano hayo yatashirikisha wanariadha kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Canada, Marekani, Afrika Kusini na Rwanda.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments