Nimemrejesha Iddi Stars-Maximo

Hatimaye yule kiungo mahiri wa Klabu ya Yanga Athuman Iddi, afurahishwa kurejeshwa tena kwenye kikosi cha taifa ‘Taifa Stars’.

Kikosi hicho cha Stars kinatarajia kupambana na kikosi cha Malawi, katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa itakayo sheheni hapa hapa kwenye ardhi ya nyumbani.

Kiungo huyo ambaye hapo awali alikuwa tegemezi ndani ya kikosi cha kwanza cha Marcio Maximo, na alishindwa kucheza ligi na kuachwa na Kocha wa timu hiyo kutokana na mgogoro wake wa uhamisho kutoka Simba kwenda Yanga.

Nyota huyo alilazimika kukaa nje yapata miezi mitatu kutokana na hatia ya kutaka kumpa kichapo mwamuzi, kwa sasa si Iddi wa zamani bali ni Iddi mpya kwani amekuja na moto mwingine pia.

Iddi ameibuka kwa kuonyesha kiwango safi katika mechi tatu, alipoiongoza yanga kuishinda Ashanti United kwa mabao 2-1 katika mchezo uliotawaliwa na ubabe.

Alisema anawashukuru sana kuweza kuteuliwa tena katika kikosi cha Maximo, kwani kochahuyo ameweza kutambua wake katika timu hiyo.

Mchezaji huyo ambaye aliweza kuchanika juu ya jicho katika mechi hiyo dhidi ya Ashanti.

Alisema katika Mechi ya Ijumaa lazima waibuke na ushindi, na mechi zitakazobaki tunataka kunyakua ushindi kwani anataka yeye awe mmojawapo wa wachangiaji wakubwa katika ubingwa huo.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments