Ghana yatolewa jasho na Guinea

Ghana walilazimika kusubiri hadi dakika za mwisho kabla ya kuilaza Guinea mabao 2 kwa 1 katika mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika, mjini Accra.

Nchi kumi na sita zinashiriki katika mashindano hayo.

Mchezaji wa Black Stars, Sulley Muntari alitimua kombora kutoka futi 25 hadi wavuni ikiwa zimesalia dakika mbili peke yake mechi kumalizika.

Hivyo basi mshambulizi huyo ambaye pia huchezea kilabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Portsmouth akaiondolea aibu nchi yake ambayo hapo awali iliichukulia Guinea kuwa mteremko.

Black Stars walikuwa wa kwanza kupata bao wakati Asamoah Gyan alivuna penalti mnamo dakika ya 54.

Lakini Guinea walionyesha machachari na usumbufu kiasi cha kusawazisha kupitia Oumar Kallabane.

Habari hii kwa hisani ya Bbc London.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments