Ligi Kuu yasogezwa mbele Tanzania

Shirikisho la soka la Tanzania (TFF) limesogeza mbele ratiba ya mzunguko wa pili wa mechi za Ligi Kuu ya soka ya Tanzania bara, ambayo awali ilipangwa kuanza kuchezwa Januari 12 kutokana na maombi ya mdhamini.

ashley_cole_francesc_fabregas_tangle_arsenal__611715.jpg

Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa mdhamini mpya wa ligi hiyo, kituo cha televisheni cha GTV kiliomba kupatiwa historia za klabu zote zinazoshiriki tangu zilivyoanzishwa, wachezaji na namba za migongoni wanazovaa wakati wa michezo.

Mwakalebela alisema kuwa tayari maelezo hayo wamepewa viongozi wa timu hizo katika kikao kilichofanyika juzi kwenye ofisi za shirikisho hilo na kukubaliana kutekeleza majukumu waliyopewa kwa muda usiozidi wiki nne.


Alisema kuwa kutokana na maelekezo hayo mapya, mzunguko huo wa pili unatarajiwa kuanza ndani ya wiki nne zijazo.

“Tumefurahishwa na uongozi wa Moro United, ambapo leo (jana) asubuhi umeleta kila kilichohitajika na tunawaomba viongozi wengine waige mfano huo,“ alisema Mwakalebela.

[zoomer]48|500|0|picha|0|0[/zoomer]

Aliongeza kuwa kutokana na mkataba mpya waliosaini na GTV, klabu zinatarajiwa kupata Dola za Marekani 300,000 kwa ajili ya kuongezea zawadi, gharama za usafiri, vifaa na maandalizi ya mechi hizo za kumalizia ligi.

Alisema kuwa kuanzia msimu ujao ndio GTV watatoa Dola za Marekani 600,000 na wanaamini kuwa sasa hivi klabu zitaweza kuandaa timu zao vizuri ukiunganisha na fedha zinazotolewa na wadhamini wakuu ambao ni kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.

Alisema pia klabu zote zimeelezwa kuwa kila moja itaonyeshwa moja kwa moja katika televisheni si chini ya mechi mbili.

Wakati huo huo, Mwakalebela alisema kuwa klabu tatu, ambazo ni Ashanti United, Kagera Sugar na Pan African ndio hazijawasilisha usajili wake wa timu za vijana na hazitaruhusiwa kuanza mzunguko wa pili bila ya kukamilisha zoezi hilo.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments