Taifa stars…Huzuni..Huzuni kubwa!!

Timu ya taifa ya Tanzani, Taifa Stars, jana iliwahuzunisha Watanzania baada ya kufungwa bao 1-0 na kuzima kabisa ndoto za kucheza fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Ghana mwakani.

Stars, ambayo ilihitaji ushindi na kuombea Senegal itokea sare au kufungwa na Burkina Faso ili iweze kupata tiketi ya Ghana, ilijikuta ikifungwa bao hilo katika dakika ya kwanza na kuzima matumaini ya ushindi.

Wakati Stars ikitolewa jasho, Senegal imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1 na hivyo kufuzu kwenda Ghana kutoka katika Kundi la Saba.

Bao lililoizamisha Stars lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa Msumbiji, Dario Monteino na kushindwa kabisa kufanya yale yaliyofanywa kwa mara ya mwisho miaka 27 iliyopita wakati Stars ilipofuzu kucheza fainali hizo huko Lagos, Nigeria.

Kwa Mara ya kwanza taifa Stars ilishiriki michuano hiyo mwaka 1980 iliyofanyika jijini Lagos nchini Nigeria, wakati huo ikifundishwa na Joel Bendera (Mb), ambaye sasa ni naibu waziri wa michezo

Bao hilo lilipatikana baada ya beki ya Stars kushindwa kumzuia Tico Tico anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini na hivyo kumpasia Dario aliyeunganisha mpira moja kwa moja wavuni.

Stars iliingia uwanjani saa 1:13 usiku, wakati kocha Marcio Maximo aliingia saa 1:17, Rashid Kawawa kaingia 1:29.
Stars: Ivo Mapunda, Mecky Mexime, Amir Maftaha, Nadir Haroub, Salum Swedi, Henry Joseph, Nizar Khalfan, Shaban Nditi, Hatuna Moshi, Said Maulid, Abdi Kassim.

Kwa wapenzi wa michezo tunamasikitiko makubwa sana kufuatia matokeo haya, na wengi wetu tunajiuliza maswali mengi, je umefika wakati sasa Mhe Rais Jakaya Kikwete, kuelekeza nguvu na msaada kwa michezo mingine kama Riadha, Ngumi, Volleyball nk?
Wadau wengi wamekuwa na wasiwasi kuwa huko tuendako, inaonekana kama vile tuna wizara ya Mpira wa miguu zaidi, kuliko wizara ya Michezo.

Safari ta Taifa stars ndio imefikia mwisho katika mashindano haya ya Afrika, tugange yajayo na hii ni pamoja na kupata maelezo ya kitaalamu juu ya goli la dakika ya kwanza ya mchezo lililodumu kwa zaidi ya dakika nyingine 90!!

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments