MWANASOKA BORA WA AFRIKA

*BBC yatoa orodha ya watano hadharani

*Elewa jinsi ya kumpigia kura umtakaye

 

Wachezaji watano watakaowania Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2013 wamechujwa na Shirika la Utangzaji la Uingereza (BBC).

Yaya Toure wa Ivory Coast anayechezea Manchester City ameingia kwa mwaka wa tano mfululizo na anaungana na Wanigeria Victor Moses na John Mikel Obi wa Chelsea. Moses yupo Liverpool kwa mkopo wa msimu mzima.

Wengine ni Jonathan Pitroipa wa Burkina Faso anayekipiga Rennes ya Ufaransa na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon anayechezea Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Aubemeyanga aling’ara sana akiwa na St-Etienne kabla ya Wajerumani kumwona na kumchukua majira ya kiangazi mwaka huu wakati Pitroipa aliwika kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika na kuwa mchezaji bora huko, na sasa anaibeba Burkina Faso kwenye kufuzu Kombe la Dunia 2014.

Mshindi ataamuliwa na washabiki wa soka wa Afrika, ambao wana muda hadi saa 3.00 usiku wa Novemba 25 kumpigia kura chaguo lao.

Kura hizo zinapigwa kwa kupitia Newsday au kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi – sms – kwenda namba +447786202008, ambapo simu moja inaruhusiwa kutuma ujumbe mmoja tu, kwa maana ya kuchagua jina moja.

Matokeo yatatangazwa Desemba 2 mwaka huu saa 2:35 jioni kupitia kipindi cha BBC’s Focus on Africa, kwenye redio na televisheni.

Hakuna mchezaji kati ya hawa waliochujwa kutokana na orodha iliyoandaliwa na waandishi 44 wa Afrika aliyewahi kushinda tuzo hiyo kabla.

Kadhalika, Pitroipa na Aubameyang ni wachezaji wa kwanza kuchaguliwa kutoka nchi zao hizo za Burkina Faso na Gabon.
20131112-083431.jpg

20131112-083443.jpg

20131112-083456.jpg

20131112-083507.jpg

Comments