in , , , ,


SIMBA YAGOMA KUKATWA MKIA SOKOINE-MBEYA

Mchezo uliokuwa ukisubiriwa na wapenzi lukuki wa soka Tanzania bara kati ya Mbeya city na Simba sc, umemalizika katika dimba la Sokoine kwa timu hizo kufungana magoli 1-1. Mbeya city ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 14 ya mchezo kwa mkwaju wa penati ambayo ilipigwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji wa timu ya Mbeya city Deogratias Julias baada ya kiungo wa simba kuunawa mpira eneo la hatari.

Klabu ya simba na yanga zimekuwa zikipata faida kubwa sana ya mashabiki pale wanapocheza uwanja wa nyumbani na hata pale zinapokuwa ugenini.Hali ni tofauti sana pale timu hizi zinapotua uwanja wa Sokoine Mbeya kumenyana na timu “pendwa” ya Mbeya city. Ukianzia kwa kina mama, vijana, watoto wa shule wote wamekuwa wakiiunga mkono mbeya city kwa kiasi kikubwa kitu ambacho simba na yanga kinawafanya wawe kwenye wakati mgumu sana wanapotua Uwanja wa Sokoine.

Ujio wa mbeya city kwenye jiji la Mbeya umesaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha pindi timu kubwa kama Simba,Yanga. Azam fc na nyinginezo zinapokuja Mbeya. Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Mbeya kama vile Tukuyu, Kyela, Tunduma ambao wanakuja kuishangilia timu yao ya Mbeya city. Ujio wa watu hao ni neema kwa kina Mama Ntilie, watu wa Boda boda na hata wamiliki wa nyumba za kulala wageni.

Kuanzia majira ya saa 4, watu walianza kuingia uwanjani lakini kwa sababu watu wengi bado hawana tamaduni za kwenda mapema viwanjani, majira ya saa 8 ndipo utitiri wa watu ulianza kumwagika kwenye dimba la Sokoine.Tiketi ziliuzwa kwenye mazingira mazuri ingawa wapo wajanja ambao walilangua tiketi hizo kwa bei ya shilingi elfu tano na baadae, waliziuza kwa shilingi elfu saba.

Vituko havikosi kwenye uwanja wa Sokoine. Baada ya kushuhudia ndege wengi wakiruka juu ya goli la Yanga na kukamatwa kwa mayai matatu katikati ya uwanja wa Sokoine kwenye mechi ya mbeya city na yanga, jana simba wametoa mpya ya mwaka. Walitanguliza gari lenye mashabiki wao huku watu wakidhani ndiyo timu imeingia na baada kama ya dakika thelathini, wachezaji wa Simba waliingia kwa mguu huku wakikatika katikati ya uwanja.

Nao mbeya city walitoa kali ya mwaka kabya ya kuingia uwanjani kila mchezaji alikanyaga mstari wa uwanja mara nne na kuomba Dua ndipo akaingia. Inasadikika kulikuwa na dawa za kienyeji ambazo zilikuwa zimemwagwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo wachezaji na kutokana na hilo, timu zote zikagoma kuingia uwanjani na kufanya mchezo uchelewe kwa nusu saa. Badala ya kuanza saa 10, ulianza saa 10:30.

Matukio ya watu kuruka uwanja nayo yalijitokeza ambapo mashabiki wengi wanaosadikiwa kuwa wa mbeya city, waliruka uwanja na pamoja na askari kuwepo hakuna aliyekamatwa na kila aliporuka shabiki aliyevaa jezi ya mbeya city alionekana kushangiliwa na mashabiki hao lukuki kama shujaa!

Kindi cha kwanza kilitawaliwa sana na Simba huku kiungo Jonas Mkude na Saidi Ndemla wakionekana koelewana sana. Ramadhani singano bado alionekana kusumbua upande wa kulia alikocheza huku kushoto, akianza Haruna chanongo. Katika hali iliyowashangaza wengi, fundi wa mbeya city Mwagane Yeya alianzia benchi huku safu ya ushambuliaji ya mbeya city ikiongozwa na Paulo Noga na Deogratius Julius.

Simba walionekana kutulia sana na kutumia uzoefu wao kuweza kuwakabili vijana hao wa Mbeya city ambao kwa kiasi kikubwa walionekana kucheza wakiwa na presha ya kupata matokea.Kiungo Steven Mazanda wa mbeya city alirejea kwenye kikosi hicho cha kocha Juma Mwambusi ingawa hakuwa kwenye ubora wake ambao wengi tumezoea kuona ukionyesha ufundi wa hali ya juu katikati ya dimba.

Kocha Rogarusic wa simba alifanya mabadiliko ya kikosi chake kilichoanza ambapo golini aliaanza Yew Berko badala ya Ivo mapunda huku Henry Joseph akianza kama beki wa kushoto badala ya Issa Rashidi ambaye tumemzoea. Kocha hakuwa na papara zake za kufanya mabadiliko ya haraka pale tu mchezaji wake anapofanya kosa moja kama kawaida yake kitu ambacho niliona simba wakitulia na kulisaka goli ya kusawazisha.

Amis Tambwe ni aina ya mchezaji ambaye hana makeke mengi lakini anapoikutana na kipa huwa hafanya ajizi. Kipa wa mbeya city alifanya makosa kidogo mbele ya Tambwe na hapo hapo fundi huyo wa msimbazi akamuadhibu kwa kuupeleka mpira wavuni. Mpaka sasa Amis Tambwe anaendelea kuongoza kwa mabao ya ligi kuu Tanzania bara kafikisha jumla ya magoli 14.

Mbeya city wanastahili heshima kwenye mbio hizi za kuwania Ubingwa na nafasi mbili za juu kwenye msimamo ambazo zinaifanya timu kuweza kushiriki michuano ya Afrika. Wanafanya kile ambacho mashabiki wao wanakitaka na kuwaamini. Kila kona ni mbeya city tu kuna muda nashangaa kwa nini watu wa Kigoma wanalia pale Simba au Yanga wanapofungwa wakati wana timu yao ya JKT kanembwa na hawaipi ushirikiano!

Mpaka dakika tisini za mchezo zinamalizika,Mbeya city 1-1 Simba na kiukweli, pongezi ziwaendee waamuzi wa mchezo. Mchezo wa soka uko kwenye kasi sana na ndiyo maana hata Ulaya wanajaribu kuanza kutumia Tekinolojia ili imsaidie mwamuzi. Hapa kwetu waamuzi wetu wanajitahidi sana ila ni nadra sana kuona wanasifiwa!.
Imeandikwa na Oscar Jn

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Okwi ruksa Yanga

Man City wawapiga Chelsea