in , , ,

Tanzania Kucheza Nusu fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani, Brazil…

Timu ya Taifa ya Tanzania ya watoto wanaoishi mitaani – Tanzania Street Star kwa mara nyinginge imeweza kufika katika nusu fainali za mashindano ya Kombe la Dunia kwa vijana wanaoishi mitaani ( Street Child World Cup 2014) yanayofanyika kwa mara ya pili toka kuanzishwa na safari hii yakifanyika katika Jiji la Rio de Janeiro.

Tanzania leo imeweka kufika fainali baada ya kuifunga moja ya timu ngumu kabisa katika mashindano haya timu ya Indonesia kwenye mechi ya Robo fainali iliyochezwa majira ya asubuhi hapa Rio de Janeiro.

Katika mechi hii ya robo fainali Tanzania ilikuwa ya kwanza kupachika magoli ya mapema katika kipindi cha kwanza yakifungwa na Michael pamoja na Hassan. Baada ya magoli hayo Indonesia waliweza kuishambuli Tanzania kwa takribani muda wote wa mchezo wakisaka kurudisha magoli. Indonesia waliweza kusawazisha magoli katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza na mwanzoni mwa kipindi cha pili na kuufanya mchezo kumalizika kukiwa na sare ya magoli mawili kwa mawili hivyo kulazimika kucheza muda wa nyongeza ambao pia ulimalizika magoli yakiwa mbili kwa mbili. Kufuatia matokeo hayo na sheria za mchoze wa wachezaji saba uwanjani ( 7 aside) ziliamuliwa penati kupigwa. Penati 3 ziliamuliwa kupigwa kwa kila timu na Tanzania ikafunga penati 3 Indonesia ikafunga 1 na kufanya matokeo ya mchezo kuwa 5 kwa Tanzania na 3 kwa Indonesia.

Penati za Tanzania zilipigwa na Michael, Emmanuel (golikipa) na Hassan penalt ya mwisho. Na nyota wa mchezo alikuwa golikipa wa Tanzania Emmanuel aliyeokoa michomo mikali golini kwa timu ya Tanzania. Na kuweza kuibeba timu hadi nusu fainali, Emmnauel amekuwa gumzo kweli kweli katika mashindano haya akidhaniwa kuwa ndiye goalikipa bora wa mashindano mpaka sasa.

Kwa matokeo hayo Tanzania imefuzu kwenye nusu fainali hizi na hivyo itacheza na USA katika kusaka tiketi ya kucheza fainali na mshindi wa 3 na 4 siku ya Jumapili mechi zitakazo chezwa kwenye Uwanja wa Klabu maarufu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro. Timu nyingine zilizoingia nusu fainali na mechi zake zitachezwa kesho ni Burundi vs Pakistani, timu hizi mbili pamoja na USA zimesheheni vijeba, wachezaji wao wanaomekana dhahili kuwa na umri mkubwa sana kama kama U20 wetu wa Tanzania hivyo kuipa Tanzania wakati mgumu kushindana na wachezaji wenye umri mkubwa sana.

Mashindano ya mwaka huu yamekuwa magumu na makubwa sana, na ushani umekuwa mkubwa na timu kukamiana. Tanzania imekifa nusu fainali ya mashindano baada ya kucheza na timu za Burundi 2 – 2 Tanzania, Tanzania 3 – 0 Argentina, Tanzania 2 – 0 Nicaragua, Philippines 2 – 0 Tanzania, na robo fainali Tanzania 5 – 3 Indonesia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Mrundi Beraniho roho kwatu

Ferguson huyoo Harvard