in , ,

*SERIKALI YARIDHIA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF*

Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa
wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga
amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara,
TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Amesema baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato
huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea
walioenguliwa.

Rais Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee,
pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama
walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane
imetendeka.

“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu
huko ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko
tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri
mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze
kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.

Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa
na FIFA baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa
TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya
maana hata kidogo.

Hivyo amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi
na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza wao
na vyombo vilivyowaengua.

Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini
vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA
ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.

Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa
TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.

Rais Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za
wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano
ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa.

*RAIS TENGA AIPONGEZA AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO*

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
ameipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa mabao 2-1 ilioupata timu yake
katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

Mechi hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ilichezwa jijini Monrovia,
matokeo ambayo yanaweka Azam katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya
mchezo wa marudiano utakaofanyika wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Amesema Azam imefanya jambo kubwa, kwani kushinda ugenini hasa katika nchi
za Afrika Magharibi si jambo dogo, hivyo Watanzania waendelee kuiunga mkono
na anaitakia kila la kheri katika mashindano hayo.**

* *

*MSAFARA WA MOROCCO KUTUA NCHINI IJUMAA*

Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini
keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe
la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa
habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.

Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye
Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.

Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni
Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar,
Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal,
Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.

* *

Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar,
Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin
Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El
Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.

Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa
katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo,
mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha
Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.

Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili
mchana.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

*KIKOSI CHA MOROCCO KUTUA NCHINI IJUMAA*

Qatar kupokwa uenyeji Kombe la Dunia?