in , , ,

MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF

 

Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na
maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka
huu jijini Dar es Salaam.

* *

Awali mkutano wa uchaguzi ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu
lakini tukauahirisha kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA), hivyo tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano huo.

Orodha ya wajumbe iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa
kama kuna wanachama wetu wana mabadiliko ya majina ya wajumbe
watakaohudhuria wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka
huu.

Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na
klabu 14 za Ligi Kuu ya Vodacom.

* *

*WAWILI WAPINGWA UCHAGUZI WA TFF*

Wanamichezo wawili walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu
wamewekewa pingamizi.

Waliopingwa ni Wallace John Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na
Vedastus Kalwizira Lufano anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia
Kanda Namba Mbili ambayo ni mikoa ya Mara na Mwanza. Anyempinga Karia ni
Shamsi Rashid Kazumari wa Dar es Salaam wakati Lufano anapingwa wa Samwel
Nyalla wa Mwanza.

* *

Pamoja na mambo mengine, Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia mkataba
na Azam Tv wakati akijua kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina nguvu za
kisheria kusaini mkataba huo.

Naye Nyalla ambaye pia ni mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe
kupitia Kanda hiyo anampinga Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka mitano
katika uongozi wa mpira wa miguu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbezeleni
itakutana kesho (Agosti 28 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kusikiliza
pingamizi hizo ambapo wawekaji pingamizi na waliopingwa wanatakiwa kufika
wenyewe ndani ya muda kwa vile uwakilishi hautakiwi.

* *

*YANGA, COASTAL UNION KUUMANA VPL*

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya pili kesho (Agosti 24 mwaka
huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani huku macho na masikio ya washabiki
wengi yakielekezwa kwenye mechi kati ya Yanga na Coastal Union.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni
kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mwamuzi
Martin Saanya wa Morogoro ndiye atakayepuliza filimbi wakati Kamishna
atakuwa Omari Walii kutoka Arusha.

Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko
Turiani mkoani Morogoro wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora
utakuwa mwenyeji wa pambano kati ya wenyeji Rhino Rangers na Azam.

Vumbi lingine litatimka kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani
Pwani wakati maafande wa JKT Ruvu watakapokwaruzana na wenzao wa Tanzania
Prisons kutoka Mbeya. Mbeya City na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Jiji la Tanga litakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ashanti
United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Oljoro JKT itakuwa
mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid
jijini Arusha.

* *

*RATIBA COPA U15 KUPANGWA ALHAMISI*

Ratiba ya michuano ya U15 Copa Coca-Cola ngazi ya kanda mwaka huu itapangwa
keshokutwa (Agosti 29 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Michuano hiyo ya kanda itaanza Septemba Mosi mwaka huu wakati mikoa
inakumbushwa kuwa inatakiwa iwe imewasilisha usajili wa wachezaji wao
kufikia Agosti 28 mwaka huu kupitia email ya TFF ambayo ni
[email protected] na nakala kwa madadi_salum@ yahoo.com

Pia mikoa inakumbushwa kutowajumuisha wanafunzi wa darasa la saba katika
timu zao katika ngazi ya kanda na fainali itakayochezwa Dar es Salaam
kuanzia Septemba 7 mwaka huu kwa vile watakuwa katika mitihani ya kumaliza
elimu ya msingi. Timu zinatakiwa kufika vituoni Agosti 30 mwaka huu.

Kanda hizo ni Mwanza itakayokuwa na timu za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma,
Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,
Manyara na Singida inaunda Kanda ya Arusha.

Zanzibar itakuwa na Kaskazini Pemba, Kusini Pemba na mikoa miwili ya Unguja
wakati Kanda ya Dar es Salaam ina Ilala, Kinondoni, Lindi, Mtwara, Temeke
na mkoa mmoja wa Unguja.

Kanda ya Mbeya inaundwa na Iringa, Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma
wakati Dodoma, Morogoro, Pwani na Tanga zinaunda Kanda ya Morogoro.

Mwanza itatoa timu nne kucheza hatua ya fainali wakati kanda nyingine za
Arusha timu mbili, Zanzibar (2), Mbeya (3) na Kanda ya Morogoro itaingiza
timu mbili.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Manchester City hoi kwa Cardiff

Arsenal wavuka kigingi Mabingwa Ulaya