in , , ,

Liverpool fungu la kukosa

Liverpool wameendelea na biashara ya hasara baada ya kuchabangwa 3-1 na Crystal Palace katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Vijana wa Brendan Rodgers walianza vyema kwa Rickie Lambert kufunga dakika ya pili tu ya mchezo, lakini wenyeji wanaofundishwa na mkongwe Neil Warnock walisawazisha na kuongeza mabao mawili muhimu kupitia kwa Dwight Gayle, Joe Ledley na Mile Jedinak.

Liverpool sasa wamefikisha mechi tano bila kushinda yoyote, wakiwa nyuma ya vinara wa ligi Chelsea kwa pointi 18 wakati msimu uliopita walimaliza wakiwa nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City.

Ni Palace hawa hawa ambao msimu uliopita waliwapunguza Liverpool katika kasi ya kuchukua ubingwa kwa kuwalazimisha sare ya 3-3 hapo hapo Selhurst Park. Nyuso za wachezaji wa Liverpool baada ya bao la tatu Jumapili hii zilijawa huzuni na kuchanganyikiwa.

Kutokana na walivyocheza msimu uliopita, watu wengi walitarajia Liverpool watishe sana msimu huu, lakini hawana mshambuliaji aliyewaongoza, Luis Suarez aliyehamia Barcelona wala Daniel Sturridge aliyeumia na kuwa benchi kwa muda mrefu.

Kocha Rodgers amesema wapo katika hali mbaya, hawachezi kitimu, pasi zao si nzuri, hawajiamini na kwamba anabeba lawama zote na kwamba lazima atafute suluhu ya kudumu. Baadhi wanashangaa kushuka viwango kwa nahodha Steven Gerrard na mshambuliaji Raheem Sterling.

Hii ilikuwa mechi ya tatu mfululizo kupoteza, ambapo pia mshambuliaji wao mpya na mtata, Mario Balotelli hakucheza kwa sababu ameumia na alilazimika kuondoka kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Italia majuzi.

Rekodi zinaonesha kwamba katika kipindi kama hiki cha msimu, ni mwaka 1992 tu Liverpool walipata kuwa na pointi chache zaidi ya hizi, ambapo walikuwa nazo 13. Pamekuwa na maneno kwamba kocha Rodgers atafukuzwa kazi, kwa maelezo kwamba wamiliki wa Kimarekani wameanza kukosa uvumilivu.

Katika mechi nyingine Jumapili hii, wakicheza ugenini, Tottenham Hotspur walipigana kiume na kufanikiwa kuwafunga Hull mabao 2-1 kwenye mechi kali.
Kwa matokeo ya mechi za mwishoni mwa wiki, Chelsea ambao bado kufungwa hata mechi moja wanaongoza ligi wakiwa na pointi 32, wakifuatiwa na Southampton wenye 25, Manchester City wana 24 wakati Manchester United wanazo 19 sawa na Newcastle.

West Ham wanashika nafasi ya sita wakiwa na pointi 18 sawa na Swansea, wakati Arsenal, Everton na Spurs wanazo 17 kila mmoja. Stoke wanashika nafasi ya 11 kwa pointi 15, Liverpool wanaangukia ya 12 kwa pointi 14 wakifuatiwa na West Bromwich Albion na Sunderland wenye 13 kila moja.

Palace walioshinda mechi tatu tu msimu huu wanashika nafasi ya 15 kwa pointi 12 wakifuatiwa na Hull na Aston Villa wenye pointi moja pungufu yao wakati Leicester na Burnley wanazo 10 kila moja na mkiani wapo Queen Park Rangers wenye point inane tu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal nyumba ya njaa

Hamilton: Ushindi ni mwanzo mpya