in ,

Hatimaye Mwalimu wa Taifa Kikapu kuwasili leo…

Awali tulitangaza kuhusu ujio wa Makocha wa kikapu toka Marekani kuja kufundisha timu yetu ya Taifa, ambao ni Albert Sokaitis (Kocha Mkuu) ambaye ni Kocha mwenye uzoefu wa miaka 24 kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko huko Marekani katika jimbo la Connecticut. Pia amewahi kufundisha timu na kuendesha mafunzo nchi za Uchina, Lebanon, Ugiriki na Japan.

Ambaye  atasaidiwa na Kocha Jocquis L. Sconiers ambaye nae ana uzoefu wa miaka mingi na kwa sasa ni Kocha Mkuu Msaidizi wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko Marekani katika jimbo la Connecticut.


Katika utekelezaji wa mpango huo katika awamu ya kwanza Kocha Sconiers anatarajiwa kuwasili nchini leo tarehe 02/11/2012 na ataelekea Tanga siku inayofuata katika Mashindano ya Kombe la Taifa ili kuchagua wachezaji watakaonda timu za Taifa (wanawake na wanaume) na baada ya hapo ataanza mafunzo rasmi kwa timu zote  mbili tarehe 5/11/2012.  Kocha Mkuu Sokaitis atakuja nchini baadae kuungana na Sconiers ili kuendeleza mafunzo haya katika mpango  wa maendeleo ya kikapu wa miaka 4, ambao tutakuwa tunaufanyia tathimini kila baada ya miaka 2.

Awamu hii ya kwanza ya mpango wa mafunzo unadhaminiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa Tanzania, tunawashukuru sana watu wa Marekani.

Afisa wa mambo ya Umma wa ubalozi wa Marekani nchini ndugu Roberto Quiroz  ndio atakuwa mgeni rasmi katika kufungua kambi hii ya timu ya Taifa itakayofanyika katika viwanja vya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Masaki.

Tunaomba wadau wote mtuunge mkono kwa hali na mali kufanikisha mpango huu wa mafunzo kwa timu ya Taifa na kwa makocha wetu wazalendo kwa faida ya vijana wetu na Taifa letu.


Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Zanzibar National Beach Volleyball Championship ends

Orodha ya Viongozi wa Vyama vya Michezo Tanzania na Mawasiliano yao..