in , , ,

FUNGA KAZI YA USAJILI

*Falcao, Welbeck, Negredo wafunika
*Usajili umevunja rekodi kufika £835
 

Dirisha la usajili limefungwa msimu huu, habari kubwa ikiwa ni ya Radamel Falcao kutua Manchester United na Danny Wellbeck kutoka Man U kwenda Arsenal kwa mkataba wa muda mrefu.

Falcao ameingia Man U kwa mkopo wa msimu mzima na anaweza kusajiliwa moja kwa moja baada ya kipindi hicho, huku usajili mzima kwa klabu za Ligi Kuu ya England (EPL) ukifikia rekodi mpya ya pauni milioni 835.

Mchezaji huyo wa Colombia amesema kwamba atacheza kama beki wa kati, licha ya kujulikana kwamba ni mshambuliaji wa kati, hali iliyokuwa inawatia matumbo joto Wayne Rooney na Robin van Persie wanaocheza nafasi hiyo. Atakuwa analipwa kati ya pauni 190,000 na 265,000 kwa wiki.

Old Trafford wamempata Falcao wa Colombia na Monaco kwa pauni milioni sita, wakakamilisha usajili wa Daley Blind kutoka Ajax kwa pauni milioni 13.8 wakati wamemuuza Welbeck kwa pauni milioni 16.

Mchezaji mwingine muhimu wa EPL, ambaye hata hivyo alishindwa kuonesha makali, Alvaro Negredo wa Manchester City amepelekwa Valencia ya Hispania kwa mkopo wa msimu mzima. United wanashikilia rekodi ya usajili ghali zaidi Uingereza, baada ya kumpata Angel Di Maria wa Real Madrid kwa pauni milioni 59.7.

Wachambuzi wa masuala ya fedha, Deloitte, wanasema kwamba Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal ametumia pauni milioni 150 kwenye usajili na ndiyo rekodi kubwa zaidi kwa msimu kwa klabu yoyote ile.

Kusajiliwa kwa Falcao kumeshangaza wengi, kwani alitarajiwa kwenda ama Real Madrid au Arsenal alikokuwa akihusishwa sana msimu huu kabla ya dirisha kufungwa saa tano usiku wa Jumatatu hii.

City pia wamemruhusu mchezaji wa kimataifa wa England, Micah Richards kujiunga kwa mkopo Fiorentina nchini Italia wakati mpachika mabao wa United, Javier Hernandez ameenda kwa mkopo Real Madrid na kusema ndoto yake imetimia.

Hull ndio walivunja rekodi ya kusajili wachezaji wengi zaidi katika siku ya mwisho, kwani walipata wanne; mshambuliaji Abel Hernandez, Hatem Ben Arfa, Gaston Ramirez na Mo Diame.

Crystal Palace wamevunja rekodi yao kwa kumsajili winga wa Wigan, James McArthur kwa pauni milioni saba. Matumizi ya EPL yameongezeka kutokana na pauni bilioni tatu zinazopatikana kwa klabu kwa matangazo ya televisheni, zikiwa ni asilimia 70 zaidi ya mkataba uliopita.

Liverpool msimu huu wa usajili wametumia jumla ya £117, Chelsea £91.3m, Manchester City £50m, Arsenal £82m, Southampton £74.9m wakati wenyewe walipata £92m kwa kuuza wachezaji wao nyota sita.

Wachezaji wengine waliovunja rekodi ya usajili wa bei mbaya ni Alexis Sanchez aliyetoka Barcelona kwenda Arsenal kwa £35m, Diego Costa kutoka Atletico Madrid kwenda Chelsea kwa £32m, Eliaquim Mangala wa FC Porto aliyekwenda Manchester City kwa £32m, Cesc Fabregas  toka Barcelona hadi Chelsea kwa £30m.

Wachezaji wengine ni Ander Herrera toka Athletic Bilbao kwenda Manchester United kwa £29m, Romelu Lukaku aliondoka Chelsea na kujiunga Everton kwa £28m, Luke Shaw kutoka Southampton hadi Manchester United kwa £27m na dili linaweza kupanda hadi £31m, Adam Lallana wa Southampton aliyekwenda Liverpool kwa £25m Dejan Lovren wa Southampton kwenda Liverpool kwa £20m, Lazar Markovic kutoka Benfica kwenda Liverpool kwa £20m

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

TETESI ZA USAJILI LEO LEO

Welbeck aliota ataingia Arsenal