in

Mwingine aaga Olimpiki…..

Mtanzania Ammar Ghadiyal amefuata nyayo za bondia Seleman Kidunda kuaga mapema Michezo ya Olimpiki 2012 baada ya kutolewa katika raundi ya kwanza ya mashindano ya kuogelea ya mita 100 ‘freestyle’ yaliyofanyika jijini London, Uingereza jana.

Ammar ambaye, hata hivyo, ushiriki wake ulikuwa ni wa kujifurahisha kwavile hakufuzu na alicheza Olimpiki kupitia nafasi maalum za upendeleo, alishindwa vibaya jana baada ya kushika nafasi ya 57 kati ya washiriki 62 akitumia muda wa dakika 1:05.

Ammar Ghadiyal, aliyeshika Bendera ya Taifa, aaga mashindano ya Olimpiki 2012

Mashindano hayo ya awali ya wanaume yalikuwa ni ya kusaka washindi 16-Bora ambao wamesonga mbele katika safari yao ya kuwania medali.

Mwakilishi mwingine wa Tanzania, Magdalena Moshi, ambaye pia hakufuzu kama Ghadiyal, anatarajia kujifurahisha leo katika mashindano ya kuogelea ya mita 100 (wanawake).

Magdalena, kama ilivyokuwa kwa Ghadiyal, hatapewa medali hata akishinda kwa sababu hakufuzu kwa Michezo ya Olimpiki 2012 na atashiriki kupitia nafasi maalum za upendeleo zinazotolewa na shirikisho la mchezo huo duniani (FINA) kwa nchi ambazo zimeshindwa kabisa kuwa na muogeleaji hata mmoja aliyefuzu.

Baada ya bondia Kidunda kudundwa kirahisi kwa pointi 20-7 dhidi ya bondia Vasilii Belous wa Moldova katika pambano la hatua ya awali lililofanyika juzi la kusaka washindi 16-Bora, matumaini ya Tanzania sasa yamebaki kwa wanariadha wanne tu ambapo mwanadada Zakia Mrisho atachuana Agosti 8 katika mbio za mita 5,000.

Wanariadha wengine wa mbio za Marathon, Samson Ramadhan, Mohamed Msenduki, na Faustine Mussa watatupa karata zao Agosti 12.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wachache waliopewa dhamana wameshindwa kuwasaidia wananchi kuvuna asali-Tunahitaji kupokezana vijiti vya uongozi Michezoni

Ngassa milioni 80/- Awekwa sokoni na Azam Fc