TanzaniaSports.com
Karibu TanzaniaSports.com, Welcome to TanzaniaSports.com. The primary aim of www.tanzaniasports.com is to provide a forum for exchange of ideas between sports leaders, coaches, sports personalities, government and others concerned with sports, on how to improve participation and raise standards in sports in Tanzania

Archive for the Maoni Category

Man City imejisafishia njia ya ubingwa?

Posted by tanzaniasports.com on May 8th, 2012 | 1 Comment

LIGI Kuu ya Uingereza inaelekea ukingoni, huku Manchester City ikiukaribia ubingwa huo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 44.
Ushindi wa Jumapili iliyopita wa vijana hao wa Roberto Mancini ugenini dhidi ya timu ngumu ya Newcastle United umeisogeza pazuri.
Magoli mawili safi ya Yaya Toure yamemlainisha Mancini ambaye siku zote, hata baada ya kuwa na uwiano mzuri wa magoli dhidi ya United, amekuwa akisema bado mahasimu wao hao ndio wenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Kinachosubiriwa kwa hamu ni michezo ya mwisho Jumapili ijayo kati ya Manchester City watakaokuwa nyumbani Etihad kukipiga na Queen Park Rangers (QPR) wakati Manchester United wakimenyana na Sunderland kwenye uwanja wa Loftus Road.
Adui yako mwombee njaa, na Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameweka matumaini yake mikononi mwa Kocha Mkuu wa QPR, Mark Hughes aliyepata kuwa mshambuliaji wa United na pia kocha wa City.
Katika kile kinachoweza kuwa kama kichekesho, Ferguson anasema anatamani Hughes mwenyewe angekuwa anacheza katika mchezo huo muhimu pia kwa QPR wanaojaribu kujinasua kushuka daraja.
“Hatima yote ya klabu hii (Manchester United) yaweza kuwa kwenye mchezo huo, na ningetamani Sparky (Hughes) angekuwa anacheza. Mark anaijua kazi yake vyema. Alifukuzwa na City bila kuzingatia maadili na atakumbuka hilo,” anasema Ferguson.
Hughes mwenyewe anasema ingekuwa safi sana ikiwa wangekwenda Etihad na kupata pointi, kwa sababu City wanawania kombe na timu yake inang’ang’ania kubaki kwenye ligi kuu.
“Nadhani nilitazama ratiba hii nilipoanza kazi hii na nikaona kuna kitu kigumu kinakja – lakini sasa ni juu yetu wenyewe, bado tunayo fursa ya kuhakikikisha tunabaki kwenye ligi hii kwa jitihada zetu wenyewe,” anasema Hughes.
Bosi wa City, Mancini aliyetabasamu baada ya ushindi dhidi ya Newcastle kwenye mchezo mgumu ambao mabao yalipatikana kipindi cha pili, anaonyesha amejawa matumaini.
Mfungaji wa mabao hayo, Yaya Toure aliyeonekana kuzungumza kwa faragha na Mancini kabla tu ya kuanza mechi hiyo muhimu, anasema lazima wajiimarishe na kwa vile wapo nyumbani, watapata nguvu ya washabiki wao.
Mancini alimwambia Toure, kwa mujibu wa mchezaji huyo mwenyewe, lazima aweke bidii ya kipekee na kuzaa matunda (mabao) kwa sababu ni mchezaji muhimu, na baada ya kosa kosa nyingi, alipata mabao muhimu.
Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Swansea ilioupata United Jumapili haukupokewa kwa furaha kubwa, kwa sababu ulichofanya ni kurejesha msimamo uliokuwa awali – City wakiwa juu kwa tofauti ya mabao manane.
Ikiwa timu zote hizo za jijini Manchester zitashinda Jumapili, nani ataweza kufuta pengo hilo? Hakuna kisichowezekana, japokuwa inahitajika kazi ya ziada kwa mazingira ya sasa.
Itakumbukwa kwamba Manchester United ilipata kufanya maangamizi kwenye ligi kwa kuzifunga Wolverhampton Wanderers mabao 10–1 Oktoba 15, 1892.
Kadhalika iliinyuka Walsall 9-0 Aprili 3, 1895 kabla ya kurudia kipigo kama hicho kwa Darwen Desemba 24, 1898 na dhidi ya Ipswich Town kwenye Ligi Kuu Machi 4, 1995.
Haijasahaulika bado, bila shaka, jinsi ilivyoichapa Arsenal mabao 8-2 Jumapili ile ya Aprili 28 mwaka jana, lakini leo hii itaweza kufunga idadi hiyo? United ikiweza, kipi kitaizuia City nao kufanya karamu kama hiyo au zaidi kwa kasi waliyo nayo?
Nahodha Mbelgiji wa Man City, Vincent Kompany alikuwa na haya ya kusema kuhusu timu yake baada ya ushindi wa Jumapili:
“Ufanisi wa ajabu kwa timu hii. Ninayo furaha kubwa na najivunia ninapotoka uwanjani nikiwa na wachezaji hawa maarufu.”
Kwa majirani wao wa United, wote wakiitana ‘jirani mwenye kelele’, Rio Ferdinand aliyetoka mapema kwenye mechi dhidi ya Swansea alisema; “sasa mpaka mechi ya mwisho wa msimu ndipo iamuliwe ubingwa unakwenda wapi…mambo yanaendelea mpaka mwishoni mwa wiki ijayo!”
“Tulipania kushinda mechi hii iwe iwavyo na tulifanikiwa kufanya hivyo dimbani,” ni maneno ya Sergio Aguero wa City ambaye Jumapili alikuwa na kigugumizi akiwa ndani au karibu na eneo la 18.
Je, kiu ya ubingwa kwa miaka 44 itatulizwa Jumapili ijayo au United itaibuka na ngekewa na kuchukua kombe? Wakichukua City, Ferguson ameshasema kitakachokuwa kimesababisha ni uzembe wao (United) kwenye mechi dhidi ya Everton walipokubali kudhibitiwa dakika za mwisho na kutoka sare ya mabao 4-4.
Pamoja na kupata faraja kwa kufuta tofauti ya pointi nane iliyokuwepo kati ya City na United wiki chache zilizopita, Mancini anasema kikubwa ni kunyakua pointi tatu Jumapili.
“Mambo bado, ni muhimu kupata pointi tatu wiki ijayo. Tumefanya jitihada kubwa – bado kuna mchezo mmoja. QPR ni wagumu, wanapambana kuepuka kushuka daraja. Hakuna kilichobadilika, ni ama kupata au kukosa, hakuna kutegemea timu nyingine tena,” anasema Mtaliano huyo.
Man City iliongoza ligi kwa tofauti kubwa ya pointi kwa muda mrefu, kabla ya kuka kupoteza mwelekeo na kuifanya United ipande taratibu hadi kuifikia na kisha kuivuka kwa point inane.
Wakati wa masahibu hayo, City walikuwa na sintofahamu ya mchezaji wao muhimu wa Kiargentina, Carlos Tevez aliyekuwa amekosana na kocha wake baada ya kudaiwa kukataa kupasha ili aingie dimbani kucheza dhidi ya Bayern Munich Septemba 27, 2011.
Baada ya hao Teves alikosa mechi nyingi na hata kuondoka kambini na kwenda kwao Argentina bila ruhusa, kabla ya kurejea na kupatiwa adhabu, ikiwamo faini.
City ilikuwa pia na mkasa wa mshambuliaji wake Mtaliano, Mario Balotelli ambaye amekuwa na vitendo vya utovu wa nidhamu na wakati mwingine vituko vya mara kwa mara. Tangu amalize kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mechi ya ligi dhidi ya Arsenal Aprili 8, 2012, Balotelli hajacheza tena. Safu ya ushambuliaji inaonekana kuwa tishio wanaposhirikiana Tevez na Aguero, japokuwa Jumapili Tevez hakufurukuta na alitoka akaingia Edin Dzeko.
Kana kwamba ni yale ya sizitaki mbichi hizi za Sungura, Sir Ferguson alikuwa na hili wakati ligi ikielekea ukingoni:
“Tumeshatwaa kombe hili mara kadhaa kwa hiyo hata tukilikosa sijali sana, City wanapewa nafasi kubwa sana na watafanya kila wawezalo kulichukua. Matarajio na wajibu wa wachezaji wa Manchester United ni kushinda mechi. Tutakwenda pale tukiwa na matumaini. Haitakuwa rahisi lakini itabidi.”
Wakati Ligi Kuu ikitimiza miaka 20, mfalme wa soka atatangazwa kwenye mechi muhimu mbili za mwisho, ambapo mechi zote za Jumapili zitaanza saa 9.00 kwa saa za Uingereza.
info@tanzaniasports.com

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMaoni

African Champions League group places up for grabs

Posted by tanzaniasports.com on April 23rd, 2010 | No Comments

TP Mazembe of DR Congo

Mazembe continue the defence of their Champions League title against Djoliba

Reigning champions TP Mazembe of DR Congo are one of 16 sides battling to reach the group stages of the African Champions League.

The big-spending Congolese side continue their defence with a first leg game away at Mail’s Djoliba, who have never progressed beyond the third round.

The Malian side have scored just twice in four Champions League games this year and have conceded just one goal.

Mazembe should prove too strong for Djoliba over the two legs, but the likely mid-year transfer of captain and consistent scorer Tresor Mputu Mabi to a European club may weaken their challenge.

SuperSport United take on Nigerian visitors Heartland as they try to boost the image of South Africa in the African Champions League.

Orlando Pirates are the only South African side to have won the continent’s top club competition and they made a shock first round exit this year.

But SuperSport will have to do without goalkeeper Emile Baron, defenders Morgan Gould and David Kannemeyer and striker Glen Salmon through injury.

They are also missing Bongani Khumalo, who is with the national squad on a pre-World Cup training camp in Germany.

Early exits from the domestic League Cup and FA Cup competitions have not helped the club’s morale, nor have media reports linking their coach Gavin Hunt to big-spending Pretoria neighbours Mamelodi Sundowns.

Hunt longs for African success after an unexpected second round loss to KCC of Uganda last year.

Heartland, who are the sole Nigerian challengers after the surprise early elimination of Bayelsa United, suffered the heartbreak of losing the final last year to TP Mazembe on the away-goals rule in the DR Congo.

Six time African Champions Al Ahly of Egypt are without injured striker Emad Moteab as they travel to play Al Ittihad in Libya while compatriots Ismailia confront Al Hilal of Sudan in Omdurman.

Both Algerian challengers are former title holders and they enjoy home advantage first with JS Kabylie meeting Petro Atletico of Angola while Entente Setif play Zanaco of Zambia.

Fixtures between high scorers Esperance of Tunisia and Al Merreikh of Sudan in Tunis and 1998 runners-up Dynamos of Zimbabwe and Botswana’s Gaborone United in Harare complete the line-up.

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: -1 (from 1 vote)
Post Tags:
Post Categories: Maoni

Tanzania hakuna mawakala wa soka-Mgosi

Posted by tanzaniasports.com on March 21st, 2010 | 1 Comment

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema tatizo kubwa kwa wachezaji wa Tanzania kucheza soka ya kulipwa ni mawakala.

Kwa muda sasa,wachezaji wengi wa Tanzania wamekuwa wakitamani kucheza soka ya kulipwa Ulaya na sehemu nyingine duniani, lakini wameshindwa kufanikiwa kwa kukosa mawakala wa uhakika wa kutafutia timu wachezaji.

“Mawakala wetu wao hawana uhusiano wa moja kwa moja na klabu za sehemu mbalimbali badala yake wamekuwa wakiongea na mawakala wengine ili kuwahunganishia kwa timu hivyo inakuwa vigumu kidogo kwetu kupenya,” alieleza Mgosi

Aliongeza Mgosi kuwa hata hivyo idadi ya mawakala walioko Tanzania ni wachache sana kwa hiyo inakuwa vigumu kwao kumchukua kila mchezaji na kwenda kumtafutia timu ya kufanya majaribio.

Kinara huyo wa ufungaji wa Simba msimu huu alisema yeye bado ana nia ya kucheza soka nje ya nchi sehemu yoyote ile iwe Uganda, Kenya, Ulaya hata DR Congo.

“Kwa sasa kikubwa kwangu ni fedha endapo nitapata timu sehemu yoyote ambayo itanilipa vizuri nipo tayari kwenda nahitaji kukuawa kikosa zaidi, lakini tatizo ndio hilo la mawakala.”

“Siku hizi soka mtu anacheza sehemu yoyote kwa kuangalia maslahi yako, mpira ndio maisha yangu nahitaji kupata fedha zaidi kwa sasa nilikiwa na nguvu zangu,” alisema Mgosi mshambuliaji huyo mfupi na mwenye kasi.

Mgosi ambaye alikuwa hapa na timu kwa mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) hakusita kuonyesha hisia zake katika mchezo ujao wa timu ya Taifa, Taifa Stars dhidi ya Somalia unaotarajiwa kuchezwa Machi 27 jijini Dar es Salaam kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN 2011 nchini Sudan.

“Nadhani maandalizi yetu safari hii si mazuri ukilinganisha na mwaka juzi tulipofuzu, japokuwa tuna nafasi kubwa ya kushinda mechi yetu ijayo dhidi ya Somalia.

“Ndio wachezaji wote tulioteuliwa tupo kwenye klabu na wote tunafanya vizuri, lakini nadhani tulihitaji kukaa kambini muda mrefu zaidi kujiandaa na michezo hii kuliko ilivyo kwa sasa.”

Aliongeza kwa hali zetu zilivyo hawana budi kuwa na utamaduni wa kukaa kambini muda mrefu kidogo ili kutujingea kujiamini.

“Jambo lingine ambalo ningependa kuwaomba Watanzania ni kujifunza kukubali matokeo yote ya uwanjani kushinda, kushindwa na sare.

“Mashabiki wa Tanzania matokeo wanachojua wao ni kuishinda tu hakuna kingine timu ikifungwa kila mtu anawashutumu utadhani kwamba sisi tunapenda kufungwa,” alilalama Mgosi.

“Ukiangalia nchi za wenzetu mashabiki watashangilia timu yao hata kama imefungwa jambo hilo linatia moyo sana kwa mchezaji kujua kuna watu wanakuthamini.”

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: Maoni

Yanga yaaga rasmi Afrika, Simba ikipasha

Posted by tanzaniasports.com on March 2nd, 2010 | No Comments
Timu ya Yanga.

Yanga jana iliaga rasmi Ligi ya Klabu Bingwa Afrika katika kihunzi cha kwanza tu baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya FC Lupopo jijini Lubumbashi, JK Kongo, habari kutoka huko zilisema.

Akizunguza na Nipashe Jumapili kwa njia ya simu, msemaji wa Yanga Louis Sendeu alisema bao la wenyeji lilifungwa na Yaliembe katika dakika ya 76 kuipa FC Lupopo ushindi wa jumla wa mabao 4-2 wa raundi ya kwanza. Ili kusonga mbele, Yanga ilihitaji kushinda angalau mabao 2-0 baada ya kufungwa 3-2 nyumbani wiki mbili zilizopita lakini mvua iliyonyesha mchana jana haikuweka mazingira mazuri ya kufanya hivyo.

Wachezaji wa Yanga walikuwa wakiteleza mara kwa mara kutokana na uwanja kuwa na matope, alisema Sendeu ambaye alieleza pia mchezo uliamuliwa kwa haki na waamuzi kutoka Cameroon.

Kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic aliridhishwa na kiwango cha timu yake baada ya mechi hiyo, alisema Sendeu lakini “akalalamika timu haikuwa na bahati.”

Yanga inarudi nyumbani kesho Jumatatu kuendelea na harakati za kutetea ubingwa wa ligi kuu ya Bara, alisema Sendeu.

Katika mchezo mwingine wa klabu Afrika, lakini wa kirafiki, Simba iliichapa Zesco ya Zambia kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Uhuru anaripoti Faustine Feliciane.

Mchezo huo ulichelewa kuanza kwa zaidi ya nusu saa baada ya waamuzi kutaka walipwe kwanza posho yao kabla ya kufanya kazi.

Bao la kwanza la Simba ambayo inajiandaa na mechi ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika Machi 13, lilifungwa na Mike Barasa katika dakika ya 37 kwa shuti la mbali kabla ya Nico Nyagawa kuipatia la pili dakika tatu kabla ya mapumziko mabeki wa Zesco walipodhani ameotea. Zesco inayojiandaa na ligi kuu ya Zambia itakayoanza katikati ya mwezi ujao ilikwenda mapumziko ikiwa bao moja nyuma baada ya Enock Sakala kufunga kutokana na pasi ya kichwa ya Cliford Chipwalo.

Bao la tatu la Simba lilifungwa na Barasa katika dakika ya 64 kwa penalti baada ya Mohammed Kijuso kuangushwa ndani ya eneo la hatari na akaongeza lingine dakika mbili baadaye kwa shuti la mbali.

Simba: Ally Mustafa, Haruna Shamte, Jabir Aziz, Anthony Matangalu, Joseph Owino, Paul Terry, Uhuru Selemani, Nico Nyagawa, Kelvin Chile, Mike Barasa na Abdallah Seseme.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: Maoni

Tanzania needs a coach who thinks beyond Stars` training

Posted by tanzaniasports.com on January 11th, 2010 | 2 Comments

Early this week I came across a piece of information which I really would like to share with my esteemed readers. While browsing the net, I came across an impressive headline about a British soccer coach who is interested to come to Tanzania and make his contributions in developing both domestic soccer and players.

What impressed me most about this Briton who goes by the name of Stewart Hall is not his nationality but his knowledge about Tanzania’s soccer and his mission statement.

The mission statement which is in the well detailed eight page long document titled ‘Team Tanzania Football Development Document’ , says; “Our purpose is to lead and serve the whole football family in Tanzania to achieve success and integrity for the nation and the game through confident leadership and a clear vision. We will seek to establish a winning mentality by implementing a national coaching philosophy that will unite officials, coaches, and players by education and indoctrination into the ideology of “TEAM TANZANIA.”

In what he calls the ‘Statement of fact’; he points out that “To develop better players, we must first identify, train and encourage exceptional coaches who have the will and the knowledge to skillfully teach the skilful game to produce skilful players’.

What impressed me most is the Coach Education Programme which aims at designing and implementing the new raft of coaches courses – deliver the coaching philosophy from Course 1: Entry level certificate, certified by T.F.F whose target groups are Youth Leaders, Teachers, Community Workers and Ex players. In this category, the proposed syllabus will be sympathetic to young players aged 7-11 years.

He further plans to have Course 2; Certified by the England Football Association (FA) whose target groups will be Teachers, Ex Players and Existing established coaches of the various soccer clubs in the country.

This syllabus which is expected to be sympathetic to coaching young players ages 12-16 will be followed by Course 3 which will also be Certified by the FA and will also target Ex players and existing established coaches of the various soccer clubs in the country and the syllabus is expected to be sympathetic to coaching elite youth players and senior professionals.

Hall has previously visited Tanzania on two occasions. On the first occasion he was invited by the Tanzania Football Federation (TFF) in 2007 and is said to have had an audience with the TFF President, Leodegar Tenga.

The second occasion was when he visited the country along with the famous players from England Premier sides, namely John Barnes, Les Ferdinand and Warren Barton. The trio played at the National Stadium in Dar es Salaam for charity games to promote football in Tanzania.

Hall seems to be very much interested with coaching in Tanzania because he saw a lot of talents during his two visits he believes that he can help in moulding not only the best outfit the country has ever had but also help in establishing a sound base for coach education.

Now that the TFF is looking for a more effective coach to replace the outgoing Brazilian Marcio Maximo, it will be a blessing to look for a coach who thinks outside the box; beyond just coaching the national senior team; Taifa Stars so to speak.

Despite the fact that no British coach has ever made a great history when training the national team, Hall’s basic knowledge to the country’s soccer standard can help him come out with answers of the long stagnated riddle of the stunted soccer growth. Need I say more?

Syllersaid Mziray is a lecturer-cum-soccer coach

SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: Maoni

Tanzania kunufaika na Kombe la Dunia

Posted by tanzaniasports.com on September 17th, 2009 | No Comments

MKURUGENZI wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo, amesema ziara ya Kombe la FIFA la Dunia inayotarajiwa kuzinduliwa nchini hapa mnamo Novemba 19, 2009, inayoletwa na Kampuni ya Coca-Cola, itaitangaza nchi kwa kiwango kikubwa, haswa kwenye sekta ya utalii, pamoja na fursa zinazopatikana nchini hapa.

20060618042644FIFA_World_Cup_trophy

Thadeo amesema hayo kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam juzi.

Thadeo alisema kuwa ziara ya kombe halisi la FIFA la Dunia, ambayo Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA, kwa kushirikiana na Kampuni ya vinywaji Coca-Cola, inaiandaa na kuiendesha, ikiwa ni mara ya pili Tanzania kuwa moja ya nchi zitakazokuwa mwenyeji wa ziara hiyo.

Akizungumzia ziara hiyo, Thadeo alisema kwamba ni jambo zuri kwa Tanzania na kwamba ziara hiyo, itasaidia kuitangaza nchi na vivutio vyake.

ìZiara itachangia kuwahamasisha vijana wadogo wanamichezo kuongeza bidii kwenye soka kwa kuwapa matumaini kwamba hata wao siku moja wataweza kushiriki kwenye mechi za fainali za Kombe la Dunia,î alisema Thadeo.

Thadeo alizungumzia pia sababu ambazo zilichangia Tanzania kuchaguliwa kuwa moja ya nchi mbili tu barani Afrika ambazo zilipata nafasi ya kuwa mwenyehi wa Kombe hilo wakati wa ziara ya kwanza ya mwaka 2006.

Alisema kuwa wakati wa ziara ya Kombe la FIFA la Dunia, vyombo vyote vya habari duniani vitakuwa vinazitazama nchi zote za Afrika zitakazotembelewa na Kombe hilo. Vyombo hivyo vitatangaza kuna nini Afrika, watu waliopo nje ya bara hili wataweza kujifunza mengi juu ya Afrika.

ìJambo lingine ambalo ni muhimu ni kwamba ziara itautangaza uwanja wetu wa Taifa, ambao ni mpya, mkubwa na wenye hadhi ya kimataifa. Hii itaanzisha kitu kinachoitwa utalii wa michezo, yaani sports tourism, na itazihamasisha timu nyingi za nje ya nchi kuja kuweka kambi hapa kwani kwa sasa uwanja huu haujatangazwa ipasavyo nje ya nchi.

Akizungumzia manufaa ya fainali za Kombe la FIFA la Dunia ambazo zitafanyika barani Afrika (Afrika Kusini) kwa mara ya kwanza, Thadeo alisema manufaa yake kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla yatakuwa hasa katika kusaidia kukuza vipaji vya soka barani.

”Zaidi, kwa kuwa wakati huo Afrika itakuwa inamulikwa na vyombo vyote vya habari, hapa nchini nasi tutapata nafasi ya vivutio vyetu vya utalii kutangazwa, na fursa zote zikiwemo za uwekezaji, pia zitatangazwa. Jambo hili litachangia sana kukuza sekta ya utalii pamoja na nchi kwa ujumla,” alisema.

Ninawaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi wakati wa kulipokea Kombe na pia wakati wa hafla za uzinduzi na wakati wa kwenda kulitazama. Hatuna utamaduni wa fujo, sitarajii machafuko kutokea, natoa wito tudumishe amani, tuendelee na utamaduni wetu bila kupigana vikumbo,î aliongeza.

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: Maoni
I