TanzaniaSports.com
Karibu TanzaniaSports.com, Welcome to TanzaniaSports.com. The primary aim of www.tanzaniasports.com is to provide a forum for exchange of ideas between sports leaders, coaches, sports personalities, government and others concerned with sports, on how to improve participation and raise standards in sports in Tanzania

Archive for the Makala za Michezo Category

Manchester City wawamwagia sifa mashabiki Gwaride lafunika Jiji….

Posted by tanzaniasports.com on May 15th, 2012 | No Comments

WACHEZAJI na Kocha wa Manchester City wamepokea kwa furaha ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) kuwamwagia sifa mashabiki wao kwa jinsi walivyowaunga mkono.
Maandamano ya kihistoria yalifanyika mitaani kwa kikosi kizima kupita kikiwa na kombe hilo baada ya kulipigania bila mafanikio kwa miaka 44.
Sherehe hizo zilipambwa kwa rangi za bluu na kuhitimishwa kwa salamu kwenye viwanja vilivyopo katikati ya jiji, kikosi cha Man City kikiwa kwenye basi la wazi.
Kocha Mkuu wa vijana hao wa Etihad, Roberto Mancini aliuambia umati wa watu: “Tunajivunia wachezaji hawa kwa sababu wamefanya kila kitu kwa ajili yenu.”
Nahodha wa City, Vincent Kompany aliongeza: “Ni fahari kubwa kumwona kila mtu hapa, kuwa na kombe hili na sherehe, ni maajabu.”

Maelfu kwa maelfu ya mashabiki walijipanga mitaani wakati kikosi kikipita kwenye gari hilo kuelekea katikati ya jiji kuonyesha kombe lao. Kabla ya msafara huo kuanza, Kocha Mancini na wachezaji wa kikosi cha kwanza walitoa hotuba jukwaani nje ya Ukumbi wa Jiji la Manchester.
Mambo yalikuwa tofauti Jumatatu hii, kwa sababu mara nyingi Jiji la Manchester lilizoeleka kupambwa kwa rangi nyekundu – zinazotumiwa na Manchester United, ambao ni majirani na mahasimu wa Manchester City na wamekuwa wakiitana majirani wapiga domo.
Mwaka huu Jiji lilibadilika na kuwa bluu ya bahari – kutokana na maelfu ya mitandio waliyokuwa wamejifunga shingoni wadau pamoja na mabango waliyoshangiliwa na kupokewa nayo City.
Bosi huyu wa Kitaliano – Mancini – alichukua hatamu za ukocha Etihad mwaka 2009 na kuwezesha timu yake kutwaa Kombe la FA mwaka 2011, lililokuwa kama utangulizi kwa mwali wa Kombe la Ligi Kuu walilotwaa Jumapili jioni.
Kama kawaida, akiwa amevaa mtandio wake wa rangi ya bluu na nyeupe, Mancini aliwatania mashabiki wa City akisema: “Kuna baridi! Ni mwezi Mei, lakini kuna baridi!”
Kocha huyo alikuwa akirejea masahibu yaliyoikumba timu yake kwenye mchezo wa Jumapili, ambapo hadi kufikia dakika 90 za kawaida za mchezo, Manchester City ilikuwa imeshafungwa na Queen Park Rangers (QPR), huku Manchester United wakiwa wameishinda Sunderland.
Hata baada ya Edin Dzeko kusawazisha bao na kuwa 2-2, kazi ilionekana bado kuwa ngumu.
Mancini aliyekuwa akionekana kama kuchanganyikiwa, aliwaasa wachezaji wake kuharakisha kwa jinsi muda ulivyokuwa ukiwatupa mkono.
“Zilikuwa dakika tano nzuri zaidi na mbaya zaidi katika maisha yetu, ulikuwa wakati wa maajabu tulipofunga lile bao la tatu, lakini kabla ya hapo mambo yalikuwa magumu,” akasema.
Nahodha Mbelgiji Kompany, aliyefunga bao pekee na la ushindi kwenye mechi muhimu ya kubadili mwelekeo kati ya City na United Aprili mwaka huu alikuwa na haya ya kusema kuhusu dakika hizo:
“Kwa kweli tulijituma sana jana…ni hilo tu! Tulivikwa medali hizi shingoni na kupata kombe.”
Golikipa Joe Hart, ambaye amekuwa mchangiaji mkubwa wakati wote wa kampeni ya Manchester City kuutafuta ubingwa, alisherehekea kwa kuzunguka uwanja mzima baada ya kipenga cha mwisho.
Dakika za mwisho kwake zilikuwa kujituma zaidi uwanjani, akifikia kusonga mbele kusukuma mashambulizi, ikiwa ni pamoja na kurusha mpira kuhakikisha shinikizo linabaki langoni mwa adui zao.
Katika gwaride la ushindi Jumatatu, Hart ambaye pia ni golikipa wa Timu ya Taifa ya England, alirejea alivyokuwa akisema:
“Nilikuwa kama mashabiki jana. Sikuwa na cha kufanya kwenye mchezo ule (kwa jinsi mchezo ulivyokuwa wa upande mmoja kwa QPR muda mwingi) nilikuwa na kiti cha upendeleo dimbani.
“Hali ilikuwa ngumu na ya kuchanganya (dakika za mwisho) na sikudhani kwamba tungefanikisha, kwa kweli najivunia vijana na kila mmoja hapa. Ni ngumu kuzuia hisia, tazama watu hapa leo. Eneo lile (Etihad) lilikuwa likitetereka Jumapili nami nilitetemeka, unapoteza udhibiti katika hali kama ile. Ilikuwa moja ya siku za aina yake katika maisha yangu, na pengine moja ya siku nzuri zaidi pia.
Mshambuliaji wa City, raia wa Argentina, Sergio Aguero ndiye aliyekata mzizi wa fitina kwa kupachika bao la tatu, la ushindi na kuleta ubingwa Etihad. Alifunga baada ya kusogezewa mpira na Mwitaliano mtata Mario Balotelli aliyekuwa ameanguka chini, kisha kuambaa nao kabla ya kumwangalia golikipa na kuutumbukiza kimiani.
Huyu anakijua Kiingereza kwa mbali sana, kwa hiyo katka sherehe za Jumatatu alichoweza kufanya ni kutabasamu mbele ya mashabiki na kusema: “Asanteni sana! Nililia kidogo (nilipofunga bao lile)” Mchezaji mwenzake wa City na timu ya taifa ya Argentina, Pablo Zabaleta alionekana kueleza kilicho ndani ya moyo wake akisema:
“Nilikuwa na imani kwa asilimia 100 kwa Sergio (Aguero) wakati ule, nilijua angefunga. Najivunia timu hii, nawashukuru sana mashabiki, kwa sababu wana uwezo na wanatisha. Asanteni.”
Naye Dzeko aliyesawazisha bao dhidi ya QPR baada ya kuingia kipindi cha pili, anasema kwamba matukio ya Jumapili ni ishara wazi ya mafanikio yake katika soka hadi sasa.
“Hiyo ndiyo ilikuwa mechi kali zaidi niliyopata kucheza, na hii ni kwa hakika. Tulishafungwa mabao 2-1 na nilikuwa na dakika 25 kwa hiyo nikajaribu kila nilichoweza kuubadili mchezo. Mwishowe nikafanikiwa, nadhani tunastahili kabisa kuwa mabingwa,” akasema raia huyo wa Bosnia.
Ama kwa upande wa mlinzi wa Timu ya Taifa ya England, Joleon Lescott ambaye upigaji wake mpira wa kichwa kwa udhaifu kuelekea langoni mwake uliiwezesha QPR kupata bao la kwanza, Jumatatu alikuwa amekaukiwa sauti.
Alichoweza kuuambia umati wa mashabiki ni: “Haijalishi nini kilitokea kwa kichwa kile, tulishinda.”
Mchezaji mwingine wa Timu ya Taifa ya England, James Milner, anasema ilikuwa kama shubiri kuutazama mpira ule wakati mambo yakiwaendea mrama.
“Kupitia yote hadi kufika mwisho ni maajabu. Hali ilivyokuwa pale kwenye benchi…nilikaribia kuanguka kwenye ngazi kuwaendea vijana dimbani. Zilikuwa dakika 10 za maajabu ya kuhitimisha msimu huu wa aina yake,” akasema mchezaji huyo wa akiba ambaye hakutumika Jumapili.
Milner aliahidi kujaribu kuhakikisha kwamba msimu huu wa 2011/12 unakuwa mwanzo tu wa mafanikio endelevu kwa Manchester City.
“Tunatumaini kwamba huu ni mwanzo wa mengi. Tulikuja hapa kutwaa kombe hilo na tumefanya hivyo. Tutafurahia siku hizi chache zijazo, lakini kikubwa ni kuhakikisha taji linabaki kwa sisi kushinda tena na tena. Tunacho kikosi na klabu na mashabiki wa kufanya hivyo,” akasema Milner.
Ama kwa upande wa mshambuliaji wa pembeni, Adam Johnson, aliwasifu mashabiki wa City kwa jinsi walivyowaunga mkono miezi yote hii.
“Kila tulichofanya kimekuwa kwa ajili ya mashabiki. Tulitwaa vikombe vichache katika miaka kadhaa iliyopita. Ni jambo zuri kulipa fadhila kwa mashabiki kwa vikombe, wamesubiri miaka mingi,” akasema Johnson.
City ilitwaa taji katika mazingira magumu, ambapo ilikuwa inafungana na United kwa pointi, japokuwa yenyewe ilikuwa na uwiano mzuri wa mabao.
Hata hivyo ilikuwa ikikabiliana na QPR iliyokuwa ikipigana isishuke daraja, lakini ni timu ambayo imepata kuadhiri vigogo wa EPL.
United kwa upande wake ilikuwa ikicheza na Sunderland ambayo haikuwa na kikubwa cha kupoteza wala kupata zaidi ya heshima tu.
info@tanzaniasports.com

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMakala za Michezo

Milima na Mabonde Soka ya Uingereza

Posted by tanzaniasports.com on May 10th, 2012 | No Comments

Mengi yametokea kwenye msimu huu wa Ligi Kuu na Ligi ya Taifa ya Soka nchini Uingereza na hakika ni sawa na milima na mabonde.
Matukio ya kila namna yalihusisha klabu na timu zao zinazoingia dimbani, waamuzi, chama cha soka, wamiliki bila kusahau kwa namna ya pekee makocha na wachezaji wao.

Hawa ndio wanaopeperusha bendera ya klabu husika uwanjani; kuwapa raha au sononeko washabiki wao na hatimaye ndio mara nyingi hupongezwa au kutupiwa lawama kwa mwenendo wa timu.

Kama ilivyo kwa baadhi ya mashindano na ligi kwingine duniani, hii ya Uingereza huhitimishwa kwa kupata wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya kimataifa, lakini timu tatu zinazofanya vibaya hushuka daraja na nafasi zao kuchukuliwa na nyingine tatu kutoka daraja la chini.
Katikati ya kupanda na kushuka daraja, mambo mengi hutokea, vikiwamo vibweka aina aina, ambapo vyombo vya habari havibaki nyuma kuvidaka na kuujuza umma.
Kwa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), timu tatu zinazomaliza zikiwa juu kwenye msimamo wa ligi hupata nafasi moja kwa moja kuingia mashindano ya kimataifa.
Timu inayoshika nafasi ya nne hulazimika kuingia kwenye hatua za mchujo kabla ya inayofanikiwa kuungana na zile tatu kwenye hatua za makundi.
Chelsea kwa hali ilivyokuwa hadi mwanzoni mwa wiki, ingeweza kuingia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa njia mbili.
Ya kwanza ni ya wote – kumaliza kwenye nafasi nne za juu, lakini sasa haiwezi kwani kwa pointi ilizo nazo imegota katika nafasi ya sita hata ikishinda, kushindwa au kutoka sare kwenye mchezo wake wa mwisho Jumapili dhidi ya Blackburn.
Kete ya pili iliyobaki mkononi mwake ni kuishinda Bayern Munich ya Ujerumani katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye mechi itakayofayika mjini Munich, Ujerumani Mei 19 mwaka huu.
Vyovyote itakavyokuwa, kuna timu mbili tu hadi sasa zenye uhakika wa kushiriki michuano hiyo ya kimataifa, na zote ni za Jiji la Manchester – Manchester City na Manchester United, zinazoshika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa mtiririko huo. Hizi zinafungana kwa pointi, kinachosubiriwa ni tofauti ya uwiano wa mabao hiyo Jumapili siku pazia la Ligi Kuu ya Uingereza linapofungwa.
Ushindi au uwiano mzuri wa mabao kwa Manchester City utamaanisha kwamba itatwaa taji la Ligi Kuu ya Barclays na hayo yatajulikana baada ya mechi yake inayofanyika nyumbani dimba la Etihad dhidi ya QPR.
Ikiwa hivyo, City ambayo haijatwaa kombe hilo kwa miaka 44, itawapokonya kombe hilo mahasimu na majirani wao – United. Mabingwa watetezi hao wanamaliza msimu ugenini kwa kukipiga na Sunderland.

Washika bunduki wa London, Arsenal, ambao kwa muda sasa wanashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi itajihakkishia ushiriki wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya ikiwa watashinda mchezo wake wa mwisho ugenini dhidi ya West Brom inayofundishwa na Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Roy Hodgson.
Ama kwa upande wake, washindani wengine wakubwa kwenye ligi hii, Tottenham watajihakikishia nafasi ya nne kama wataishinda mechi yao inayofanyika nyumbani dhidi ya timu ngumu ya Fulham.
Klabu za England zina nafasi tatu kwenye Europa League zinazokwenda kwa washindi wa Kombe la FA ambao ni Chelsea; mabingwa wa Kombe la Carling – Liverpool na timu itakayoshika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu.
Ushindi wa Chelsea kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 19 utamaanisha nini? Ni kwamba klabu hiyo ya Stamford Bridge itaingia moja kwa moja kwenye hatua za makundi za ligi hiyo msimu ujao.
Hiyo haitakuwa bure, bali kwa gharama ya kuipokonya fursa timu itakayokuwa imeshika nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya England, timu ambayo sasa itapelekwa kushiriki Europa League.
Ama ushindi wa Chelsea kwenye Kombe la FA unamaanisha kwamba ikiwa haitatwaa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani wataingia kwenye Europa League kama washindi wa washindi wa kombe la FA.
Liverpool ilikuwa timu ya kwanza nchini Uingereza kufuzu ushiriki wa ligi barani Ulaya kwa kushinda Kombe la Carling. Liverpool ilifanikiwa pia kufika fainali ya Kombe la FA, lakini ukiacha hayo, haikuwa na msimu mzuri, huku ikishindwa kuonyesha cheche mbele ya mashabiki wake nyumbani Anfield, kabla ya kuwatuliza Jumanne Mei 8 kwa kuikung’uta Chelsea 4 – 1 katika mchezo wa Ligi Kuu.
Nafasi nyingine zilizotarajiwa kupatikana ‘zimeyeyuka’, kwani Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) limetoa nafasi tatu kwa Norway, Finland na Uholanzi kupitia kapu lake la Kuzingatia ‘Fair Play’. Hizo ni nafasi zinazotolewa na shirikisho hilo kwa vyama vya soka vya nchi kutokana na mazingatio hayo, navyo huzitoa kwa klabu zenye hadhi hiyo lakini ambazo hazikufanikiwa kupata nafasi ya ushiriki kwenye mashindano ya Uefa.
Timu tatu zinazoshika mkia kwenye Ligi Kuu zinashishwa daraja kwenda kwenye ligi ijulikanayo kama Champions.
Timu ya kwanza kujisogeza kwenye kushuka daraja ni Wolverhampton Wanderers iliyopoteza rasmi matumaini ya kubaki Ligi Kuu tangu Aprili 22 mwaka huu, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Manchester City. Blackburn Rovers iliungana nayo Mei 7 pale ilipokubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa timu isiyotabirika ya Wigan.
Timu nyingine iliyo katika hali ngumu ni Bolton, ambayo kwa uwiano wake wa mabao, itashushwa daraja isipokuwa kama itaishinda Stoke kwenye mechi yake ya mwisho huku ikiomba QPR ifungwe na Manchester City.
Ikiwa QPR itatoka sare na City, itabidi Bolton ishinde kwa idadi ya mabao tisa au zaidi ili ivuke idadi iliyo nayo QPR na hivyo kukiepuka kikombe cha kushuka daraja.
Aston Villa haipo mbali sana na eneo la hatari, lakini uwiano wake wa mabao unaiacha salama, kwani idadi yenyewe ni 17 ikilinganishwa na Bolton.

Ligi ya Taifa

Tukiingia kwenye Ligi ya Soka ya Taifa, maarufu kama Championship, mambo si haba, kwani pamekuwa na minyukano si kidogo.
Hii ni ligi inayoshirikisha timu 24, lakini ni tatu tu kati ya hizo zinazopanda kuungaa na vigogo kwenye Ligi Kuu. Timu mbili za kwanza zinaingia moja kwa moja, ile ya kwanza ikiwa ni bingwa, huku timu ya tatu hadi ya sita huingia kwenye mchujo ili kupata timu moja itakayoungana na zile mbili za kwanza.
Reading walikuwa timu ya kwanza kusherehekea kupanda daraja hadi Ligi Kuu, na walifanya hivyo wakiwa na michezo miwili mkononi, na kutwaa ubingwa siku nne baadaye.
Walijihakikishia kurejea Ligi Kuu Aprili 17 baada ya kuifunga Nottingham Forest bao 1-0 na wakiwa wametulia, wakatwaa kombe baada ya wapinzani wao wa karibu, Southampton kufungwa mabao 2-1 na Middlesbrough.
Hata hivyo, Southampton walikuja kutwaa nafasi ya pili, hivyo kujihakikishia kuingia Ligi Kuu moja kwa moja baada ya kuipa kipondo timu ya Coventry kwa mabao 4-0 katika mechi ya mwisho wa msimu.
Wapiganaji wengine waliopata kuwa katika Ligi Kuu, West Ham United wamekuwa wakihaha kufa na kupona kufanya marejeo hadi kufikia fainali ya mtoani baada ya kuichakaza Cardiff jumla ya mabao 5-0 kwenye mechi ya kwanza na ile ya marudiano ya nusu fainali.
Katika nusu fainali nyingine, Blackpool iliyokuwa na goli moja kibindoni kabla ya kuingia kwenye mchezo wake wa Jumatano dhidi ya Birmingham City, ilikata tiketi ya kucheza fainali Jumamosi na West Ham, baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Birmingham. Ilikuwa inahitaji sare yoyote ile au ushindi kufika fainali.
Kama ilivyo kwenye Ligi Kuu, timu tatu za chini ya msimamo wa Ligi ya Taifa zinashuka daraja na kwenda kucheza kwenye Ligi Daraja la Kwanza.
Kati ya 24 zilizoshiriki msimu huu, Doncaster Rovers walikuwa wa kwanza kuaga michuano hii yenye ushindani mkubwa baada ya kufungwa mabao 4-3 na wanyonge wenzao Portsmouth Aprili 14.
Kama wasemavyo wa sikio la kufa halisikii dawa, Portsmouth na Coventry City waliungana na Doncaster Rovers kwa safari ya Ligi Daraja la Kwanza Aprili 21. Hali hiyo ilidhihirika baada ya Doncaster Rovers kuamua kufa na mtu kwa kuwafunga Coventry City 2-0 na Derby kuwachapa Portsmouth 2-1.

LIGI DARAJA LA KWANZA

Charlton Athletic walifanikiwa kupanda daraja baada ya kuifunga Carlisle Aprili 14 mwaka huu na kutwaa taji la ligi hiyo wiki moja tu baadaye kwa kuifunga Wycombe mabao 2-1.
Nafasi ya pili kwa timu ya kupanda moja kwa moja ilichukuliwa na Sheffield Wednesday Mei 5 baada ya ushindi wa mabao 2-0 mfungwaji akiwa ni yule yule tena – Wycombe katika uwanja wa Hillsborough.
Ushindi huo wa Sheffield Wednesday uliwasukumiza wapinzani wao, Sheffield United kuingia kwenye mechi za mchujo, ambapo imepangwa kupepetana na timu inayoshika nafasi ya sita, Stevenage . katika nusu fainali nyingine, Huddersfield Town na Milton Keynes Dons zinakwaruzana kutafuta wa kuingia fainali.
Timu nne tayari zimefurushwa kwenye ligi hii na kwenda Ligi Daraja la Pili. Rochdale ilikuwa ya kwanza kuanguka Aprili 21 baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenzao waliokuwa wakichechemea, Chesterfield.

Exeter City, Chesterfield na Wycombe Wanderers ziliungana na Rochdale kwenye safari hiyo chungu n azote zilithibitishiwa tiketi ya usafiri wa kwenda huko Aprili 28. Hiyo ilikuwa baada ya Exeter City wanaopenda kujiita Grecians kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Carlisle, huku Chesterfield ikiangukia pua kwa kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Yeovil na Wycombe ikiridhia magoli mawili ya dakika za mwisho mwisho kutoka kwa Notts County hivyo kupoteza mchezo kwa mabao 4-3.

LIGI DARAJA LA PILI

Mshikemshike wa ligi hii ulishuhudia Macclesfield wakishushwa daraja Aprili 28 mwaka huu wakati
Swindon Town wakipokea tuzo na kupanda Ligi Daraja la Kwanza Aprili 21 licha ya kufungwa mabao 3-1 na Gillingham. Swindon walikuja kujihakikishia kombe baada ya kuwafyatua Port Vale mabao 5-0 wiki moja baadaye.
Waliokuwa wakishikilia nafasi ya pili, Shrewsbury Town walipanda daraja baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Dagenham & Redbridge Aprili 28. Nafasi ya tatu ilikwenda kwa timu ya Crawley Town na hivyo kujihakikishia kupanda daraja moja kwa moja kwa kuifunga
Accrington bao 1-0 Mei 5.
Katika mechi za mchujo kupata timu moja ya kuungana na hizo tatu kupanda daraja, Southend United inachuana na Crewe Alexandra, huku Torquay United ikitoana jasho na Cheltenham Town.
Timu mbili zilizokuwa zikiburuza mkia tayari zimetumwa kwenye ligi ya chini yake, ambayo sasa inajulikana kwa jina la Blue Square Bet Premier. Moja ya timu zilizoshushwa daraja ni Macclesfield Town, ambayo Aprili 28 mwaka huu ilikuwa siku yake ya mwisho ya miaka 15 ya ushiriki wa Ligi ya Soka. Habari hiyo mbaya ililetwa na kufungwa na Burton mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika nyumbani. Mei 5 ilihitimisha ushiriki wa Hereford United kwenye ligi hii, licha ya ushindi wake wa mabao 3-2 dhidi ya Torquay. Walishachelewa, kwani walitakiwa washinde mechi nyingi zaidi.

BLUE SQUARE BET PREMIER
Mashindano haya yamepewa jina la Blue Square Bet Premier kwa sababu za udhamini tu, lakini jina lake hasa ni Conference National.
Kama zilivyo ligi zilizotanguliwa kusimuliwa, inashirikisha timu za England na Wales.
Timu ya Fleetwood Town ndiyo iliyoibuka kidedea msimu huu na kupandishwa moja kwa moja kwenye Ligi ya Soka. Ilikata tiketi hiyo Aprili 14 baada ya kujihakikishia ubingwa pale wapinzani wao wa karibu, Wrexham walipotoka sare ya mabao 2-2 na Grimsby.
Kwa msingi huo, Fleetwood Town itacheza Ligi Daraja la Pili msimu ujao. Huko haitakwenda yenyewe, kwa sababu kuna timu zilizopata kucheza huko zinachuana kwenye fainali ya mtoano, nazo ni
York City na Luton Town. Hapo atapatikana mshindi wa kusindikizana na Fleetwood.
Timu nne za chini ya msimamo zimeshashushwa na nafasi zake zitachukuliwa na mabingwa na washindi wa mechi za mchujo kwenye fainali za Blue Square Bet madaraja ya Kaskazini na Kusini.
Bath City walikuwa wa kwanza katika madaraja matano ya juu kuanguka. Hiyo ilikuwa baada ya
Newport County waliyokuwa wakiifukuzia kwa karibu, kuifunga York mabao 2-1 Aprili 3.
Wanyonge hao walifuatwa na Kettering Town Aprili 7, baada ya kukandikwa mabao 3-0 na Mansfield. Wiki moja baadaye Darlington nao walianguka baada ya sare yao ya mabao 2-2 dhidi ya Bath.
Hayes & Yeading walijikatia tiketi ya kung’oka mashindanoni bila kupenda Aprili 21, licha ya ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Lincoln.
Vinara wa Blue Square Bet kwa kanda ya Kusini, Woking waling’aa Aprili 14 baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Maidenhead. Dartford inakabiliana na Welling United kwenye mchujo wa fainali Mei 13.
Hyde ilikuwa imepandishwa kwa kofia ya ubingwa wake wa Blue Square Bet kwa kanda ya Kaskazini Aprili 21 baada ya kuitungua Boston mabao 4-1. Gainsborough inaivaa Nuneaton kwenye fainali Mei 13.

LIGI KUU YA SCOTLAND
Ligi Kuu ya Scotland (SPL) iligawanyika nusu baada ya timu zote kucheza mechi 33, ambapo timu sita za juu na sita za chini zikichezeana kwenye ‘nusu zao’.
Ni hivi, baada ya mechi hizo, timu ziligawanyika kwa ubora na udhaifu au kwa vigogo na vibonde, hivyo kwamba zile sita za chini hazingeweza kwa jinsi yoyote kutwaa pointi na kupanda hadi nafasi sita za juu, kama ambavyo zile sita za juu zilishajiimarisha hivyo kutokuwa na wasiwasi wa kupoteza nafasi zao.
Mabingwa wa Scotland ni Celtic wenye pointi 90, wakiwazidi wanaoshikilia nafasi ya pili kwa pointi 20!
Rangers ndio wa pili, wakiwa na pointi 70 kibindoni. Licha ya timu 18 kushiriki Ligi Kuu ya Scotland tangu ianzishwe (timu shiriki kwa msimu ni 12), ni Celtic na Rangers tu zilizopata kutwaa taji hilo.
Lakini wakati Rangers ikisakata vyema kandanda dimbani, hali ya klabu hiyo kiuchumi si njema, kwani inatatizwa na masuala ya fedha, jambo lililosababisha kuanzishwa taratibu za kuiweka chini ya kabidhi wasii, taratibu za ufilisi zikitarajiwa kuchukuliwa, taratibu ambazo hazijajulikana zitaisha lini na kwa vipi.
Ni katika mwanga huo, Rangers imekwanza na inavyoonekana haitaweza kushiriki, hata kama ina tiketi, michuano ya Uefa kwa msimu ujao.
Ilikuwa inategema ingeondoka vipi kwenye mtanziko huo wa ufilisi, ikiwa chini ya taratibu za kisheria na iwapo ingefanikiwa kumaliza matatizo yake, kulipa madeni na kurejea kwenye uendeshaji wa klabu kama kawaida inavyotakiwa kwa klabu za soka za Scotland.
Palikuwapo matumaini makubwa kwamba klabu ingeweza kuondokana na matatizo hayo kabla ya Machi 31 mwaka huu.
Hata hivyo, akaunti za klabu hiyo haziwezi kukaguliwa na kufungwa na wakaguzi wa hesabu katika hali ya kukidhi vigezo vya wasimamizi wa soka.
Hii ni kwa sababu wanataka kuridhishwa ni kwa vipi klabu hiyo itakidhi matakwa yao kwa kuthibitisha kwamba patakuwapo ugharamiaji wa shughuli za kila siku za klabu hadi mwishoni mwa msimu ujao wa ligi.
Kutokana na ukweli kwamba hadi Machi 31 mwaka huu kabidhi wasii hakuwa akijua nani angeichukua na kuimiliki klabu, kwa hiyo hili halingeweza kupata uthibitisho ipasavyo.
Kana kwamba hiyo haitoshi, lipo jambo la tatu, nalo ni kwamba, kwa mujibu wa kanuni za Uefa, Rangers ilitakiwa iwe imeshaweka amana au kulipa madeni yote ya kodi yaliyokuwapo Desemba 31, 2011. Madeni haya kwa Rangers yanakadiriwa kuwa zaidi ya Pauni milioni tano (£5m). Kabidhi wasii hangeweza kutimiza na kuthibitisha hili.
Jambo la nne ni kwamba, klabu ilitakiwa iwe imewalipa au kuelewana na wakopeshaji wake wote kabla ya siku ya mwisho iliyowekwa ambayo ilikuwa Machi 31 mwaka huu, jambo ambalo halikufanyika.
Lakini, msimamizi wa klabu hiyo kwa sasa, Paul Clark, alisema wazi Machi 7 kwamba matakwa ya sheria na kanuni hayakuwa yanaelekea kufikiwa.
Rangers wanapojaribu kupata suluhu ya matatizo yao, Celtic wenyewe wanachekelea, wakiendelea na sherehe za ubingwa wao waliowapokonya watani wao – Rangers.
Hili ni taji la kwanza kwa Celtic katika kipindi cha miaka minne. Ilitakata kwa kuitandka Kilmarnock mabao 6-0 Aprili 7.
Wakati Rangers wakiwa na uhakika wa kumaliza wakiwa nafasi ya pili kwa vile wana pointi 70 na wanaowafuatia, Motherwell, wana pointi 62, basi nafasi yake katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya inakwenda kwa hao wanaoshika nafasi ya tatu, watakaoingia na Celtic katika raundi ya tatu ya kufuzu.
Kawaida ni kwamba timu zinazomaliza zikiwa nafasi ya tatu na ya nne hufuzu kwa Europa League pamoja na waliotwaa kombe – lakini ngekewa iliyoikuta Motherwell inamaanisha kwamba timu zitakazoshika nafasi ya nne na ya tano zitafuzu.
Hearts au Hibernian kutegemeana na atakayemshinda mwenzake, wataingia hatua za mtoano kwa ajili ya Europa League huku Dundee United wanaoshika nafasi ya nne wakiingia raundi ya tatu ya kufuzu na timu itakayoshika nafasi ya tano itaingia raundi ya pili ya mchakato wa kufuzu.
Dundee United ilijihakikishia nafasi kwenye Europa League baada ya kuifunga Celtic bao 1-0 Mei 6 wakati Hearts inatarajiwa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tano, isipokuwa kama itafungwa na Celtic katika mechi ya mwisho ya msimu huu na wakati huo huo St Johnstone iifunge Rangers.
Hata hivyo, wakimaliza ligi wakiwa nafasi ya sita, Saints watafuzu kwa Europa League ikiwa Hearts itatwaa kombe.
Kwa mujibu wa kanuni, timu inayokuwa ya mwisho kwenye msimamo wa ligi inashushwa kwenda Daraja la Kwanza, hata kama Rangers itafilisiwa. Timu iliyoshika mkia safari hii ni Dunfermline ‘The Pars’ waliohakikishia kuondoka Ligi Kuu Mei 7 baada ya kufungwa na Hibernian inayoshika nafasi ya 11 kwa mabao 4-0.

LIGI DARAJA LA KWANZA SCOTLAND

Ross County ndio mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Scotland, hivyo wamemefanikiwa kuingia Ligi Kuu ya Scotland (SPL).
Vijana hao wa Highland walijihakikishia nafasi hiyo Aprili 10 baada ya Dundee kushindwa kuwafunga vibonde wa ligi hiyo, Queen of the South ambao Aprili 28 walikata tiketi ya kushuka daraja baada ya kupigishwa kwata ya mabao 3-1 na Raith Rovers.
Ayr Club, timu inayoshika nafasi ya tisa kati ya timu 10 za ligi hiyo itaingia kwenye michezo ya mtoano na timu tatu za Ligi Daraja la Pili, kujua kama itabaki Ligi Daraja la Kwanza au itaondoka.

LIGI DARAJA LA PILI SCOTLAND
Katika Ligi Daraja la Pili nchini Scotland, msimu unaomalizika umeshuhudia Cowdenbeath wakifanya vizuri na kutawazwa wafalme wapya wa soka Aprili 21 kwa kuwafunga Forfar mabao 2-0.
Timu zilizoshika nafasi ya pili hadi ya nne – Arbroath, Dumbarton na Airdrie United zinaingia kwenye mechi za mtoano na Ayr United ya Ligi Daraja la Kwanza.
Ama kwa upande wa kushuka daraja, rungu limewashukia Stirling Albion, na uhakika wa kushuka waliupata tangu Aprili 28, walipofungwa na Dumbarton mabao 2-1. Jirani zao walioshika nafasi ya tisa nao itabidi wajitetee kwa kuingia mechi za mchujo na timu tatu za Ligi Daraja la Tatu.

LIGI DARAJA LA TATU SCOTLAND

Jitihada za Alloa Atletic zimelipa, kwani timu hiyo imetwaa ubingwa na kupanda kutoka Ligi Daraja la Tatu ilikokuwa ikicheza.
Ilichanja mbuga Aprili 7 mwaka huu baada ya kuichachafya Elgin mabao 8-1. Ili kupata timu ya pili itakayopanda, timu za Queen’s Park, Stranraer na Elgin City zitamenyana kwa njia za mtoano
Pamoja na timu ya Albion Rovers inayocheza Ligi Daraja la Pili.
Hakuna timu inayoshushwa kutoka daraja hili, japokuwa East Stirling ndiyo iliyomaliza msimu ikiwa ya mwisho kwenye msimamo.
info@tanzaniasports.com

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMakala za Michezo

Only two Tanzanian runners have so far qualified for the London Games

Posted by tanzaniasports.com on May 3rd, 2012 | No Comments

As the London Olympics is just around the corner, controversies are surfacing in connection with banned athlete Fabian Joseph.

Joseph absconded from the TOC sanctioned training camp I Kibaha and the TOC wasted no time to impose a ban and offload him from the London-bound squad for the Olympics.

The athlete has approached the Athletics Tanzania officials seeking an apology but the later told him to proceed to the TOC.

However, the TOC in turn told AT officials to apologise on the athlete’s behalf and not the other way round.

TOC secretary general Filbert Bayi said this following report that the runner met AT officials and asked them to forgive him.

Bayi said TOC want AT to apologies to the committee not the runner himself because he is directly under the athletics association.

AT president Francis John confirmed that his association met the athlete and advised him to personally apologies to TOC and then the association will do the same.

“AT met the athlete and agree to write and submit an apology letter but the athlete himself is to apologise to the committee”, he said.

The long distance runner is reportedly to have absconded from camp where he was preparing to take part in the Prague International Marathon set for

Sanctioned by the world’s athletics governing body (IAAF), the Prague Marathon will serve as the last big qualifying event for the eagerly awaited Games.

In another development, Bayi said chances are high that long distance runner Dickson Marwa might not feature in London Olympics.

Marwa left the county a week ago for Berlin Marathon but has failed to finish on the top twenty to lose qualifier bid. Bayi said he has tried to check with the athlete and also on the organizers’ website but Marwa is not even among the top thirty.

Only two Tanzanian runners have so far qualified for the London Games, Zakia Mrisho and Samson Ramadhan

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMakala za Michezo

Kijiji cha Afrika London tayari kwa Olimpiki….

Posted by tanzaniasports.com on May 1st, 2012 | No Comments

MOJA ya habari endelevu na kubwa kwa muda sasa ni ya mashindano ya Olimpiki yanayofanyika majira ya joto jijini London kuanzia Julai 27 hadi Agosti 12, 2012.
Ni mashindano makubwa yanayoshirikisha wastani wan chi 204, ambapo 165 tayari zimefuzu, huku wanamichezo wanaotarajiwa kujumuishwa wakiwa ni 10,500, na cheche zake hazitakuwa pengine zaidi ya pale Olympic Stadium, mashariki mwa jiji la London.
Afrika ambayo daima imekuwa mbele kimichezo, nyota yake iking’aa katika kona mbalimbali za dunia, inashiriki kikamilifu michezo ya mwaka huu.
Safari hii Afrika imekuja na mfumo mpya, ujirani mwema na mkakati wa pamoja kwa kuwa na Kijiji cha Afrika, kitakachokuwa eneo la makutano kwa bara lote, kusini hadi kaskazini sawa na mashariki hadi magharibi.

Wote watakutana hapo kupeana salamu, kutiana moyo na kubadilishana mawazo na maarifa ya jinsi ya kufanya vyema michezoni na kwa ujumla kulinda hadhi na sifa ya bara tukufu la Afrika.
Mipango hii imebuniwa na Chama cha Kamati za Taifa za Olimpiki za Afrika (ANOCA), mwavuli rasmi wa kamati za nchi wanachama, ulioanzishwa Lome, Togo, Juni 28, 1981.
Kwa hiyo, wakati London ikirindima kwa yote yatakayooneshwa na wanamichezo washiriki kwenye Olimpiki, Afrika inataka kuwa tofauti, kwa kuweka mbele maslahi ya eneo hilo kwa pamoja na kuhakikisha vipaji vya wanamichezo wake vinaonekana na kudhihirika.
Rais wa ANOCA, Jenerali Lassana Palenfo ambaye ni raia wa Ivory Coast, anaona ushindani mkubwa utakuwapo, kwa sababu Kamati za Olimpiki za dunia nzima zitakuwa zinajitutumua kutaka kuonyesha makali ya washiriki wake.
Kama ilivyo ada, tamu ya ushindi kwenye mashindano yoyote ni tuzo, na kwa Olimpiki kuna medali kedekede, ambapo uwaniaji wa kwanza ni zile za dhahabu, pili fedha na tatu shaba.
Afrika itaambulia ngapi? Jenerali Palenfo anasema kinachotakiwa ni kujituma, uzalendo na ari katika mazoezi, kwa sababu kama ni vipaji, tayari Afrika imeshadhihiri kuwa navyo vingi.
Hata hivyo, kando ya michezo – pengine kabla au baada ya kila tukio, kujumuika pamoja kunaijenga sana jamii ya wana Olimpiki na ni moja ya nguzo imara za kuleta ushindi kwenye hatua inayofuata.
Kijiji hicho cha Afrika ndani ya Jiji la London kipo katika eneo maarufu la Hyde Park na kitakuwa na maeneo mawili yenye majukumu yanayopandana.
La kwanza ni Klabu ya Afrika inayokuwa eneo la mapokezi rasmi lakini binafsi, mahsusi kwa ajili ya viongozi wa chama na Kamati za Olimpiki za Afrika kuwakaribisha viongozi wa michezo, wanamichezo wanaoshiriki pamoja na wadhamini wao.

Kwa maana nyingine, hili ni eneo maalumu ambalo hata zile kamati za ufundi zitapata nafasi, baraka, muda wa kuweka mambo yao sawa kwa ajili ya kuwezesha ushindi kwa wanamichezo wa Afrika.
Klabu hii ya Kijiji cha Afrika ndani ya London haitakuwa pweke wala wanaokaa humo hawapatwa ukiwa, kwa sababu kwa utajiri wa rasilimali Afrika iliopewa na Maulana, patakuwapo na studio za redio, lakini kubwa zaidi na studio za televisheni kadhalika.
Eneo la pili kijijini hapo ni Ardhi ya Afrika. Waafrika na ardhi huna cha kuwaambia, na sasa wameimega London na kutwaa ardhi yao kwa ajili ya kujitambulisha vyema mbele ya mabara na mataifa mengine.
Katika ardhi hii patakuwapo mabanda na mabango mbalimbali, yakiwakilisha utamaduni na usanii mtawanyiko unaopatikana katika Bara la Afrika.
Hawa wataonyesha mila, desturi na kwa ujumla wake utamaduni kutoka maeneo kama Afrika Mashariki, Kati, Kusini, Kaskazini bila kusahau Afrika Magharibi.
Fursa hii inatumiwa kama dirisha la Afrika kwa dunia, ambapo mabanda yatakuwa na ukubwa wa mita 16 za mraba kila moja na kuonyesha utajiri wa bara katika utamaduni.
Ardhi hii itakuwa maalumu kwa ajili ya maonyesho ya mambo ya Kiafrka na katika kukata mzizi wa fitna kwa wapendao kuonja au hata kula na kushiba, basi patakuwa na mgahawa unaotoa huduma ya vyakula vya Kiafrika.
Havitakuwa tu ni vyakula vya Kiafrika, bali ukamilisho wake ni kwamba vitapikwa Kiafrika na moshi ukilihanikiza anga la London, bila shaka ukisambaza kwa majirani harufu nzuri ya chakula kinachopikwa na kualika wengi kutoka pande tofauti. Eneo hili litakuwa wazi kwa mtu yeyote kutoka bara lolote.
Kana kwamba hiyo haitoshi, ni katika hii Ardhi ya Afrika patakuwa pia na maonyesho ya watu maalumu, walau tuseme picha za wanamichezo mahiri wa zamani wa Afrika waliowika kwenye mashindano yaliyopita ya Olimpiki na kuacha alama zisizofutika kwenye medani ya michezo.
Hizi zitakuwa picha kubwa zitakazolipamba eneo la ardhi hii, hivyo kualika watu wa asili tofauti kuivumbua Afrika na utajiri wake.
Yote tisa, kumi ni kwamba kila jioni, Kijiji cha Afrika kitarindima kwa muziki mzito wa Kiafrika kupasua anga, muziki utakaoporomoshwa moja kwa moja (live) na kundi la wanamuziki maarufu wa Afrika.
Haya ni maeneo mawili, majukwaa tofauti lakini ndani ya kijiji kimoja na yenye nia moja ya kuitangaza Afrika na yatakuwa wazi kwa watu wote muda wote wa Michezo ya Olimpiki.
Afrika inataka kutumia Kijiji cha Afrika ndani ya London kuifanya michezo hii ya aina yake kuwa sehemu ya mawasiliano muhimu yatakayodumisha udugu na urafiki, lakini zaidi kuwafunda zaidi wanamichezo kwa kuwafumbulia kwamba michezo ni zaidi ya mikwaruzano kwenye dimba.
Afrika inatarajia kushinda medali nyingi zaidi ya zile ilizopata Beijing, China mwaka 2008 na sasa inataka iunganishe nguvu kudhihirisha nguvu ya umoja, kisha kwenda kufurahia pamoja kijijini Afrika.
Kijiji hicho pia kitakachojumuisha viongozi wa michezo mbalimbali, kitatoa mwanya kwao kubadilishana uzoefu na maarifa na kupeana mbinu za kuepuka mizozo michezoni kwa waliogubikwa nayo.
Penye nchi nyingi kama hizi 53 za Afrika zinazoshiriki, patakuwa na hazina ya viongozi, wadhamini na wafadhili wenye mengi ya kuinua michezo katika Afrika na kuweka msingi imara, ili ushindi uwe daima wimbo wa Afrika.
info@tanzaniasports.com

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMakala za Michezo

Miaka 20 ya Ligi Kuu – nani mchezaji maarufu zaidi?

Posted by tanzaniasports.com on April 27th, 2012 | No Comments

Imetimia miaka 20 tangu uzinduzi wa Ligi Kuu ya England, hivyo ni wakati mwafaka kusherehekea hatua hiyo kubwa iliyofikiwa kwa Tuzo za Misimu 20.
Kwa kuzingatia miongo hiyo miwili ya ligi kubwa zaidi nchini England, Uongozi wa Ligi Kuu umewaalika mashabiki kuchagua Goli Bora, Mechi Bora, Uokoaji Bora na Ushangiliaji Bora, wakati jopo la wadau wa soka na waandishi wa habari watachagua Mchezaji Bora, Kocha Bora, Timu Bora, Msimu Bora na Nukuu ya Kukumbukwa Zaidi.

Tuzo itakayokuwa na mvuto zaidi katika kuwaniwa ni ile ya Mchezaji Bora. Wateule watakaowania tuzo hiyo ni Dennis Bergkamp, Eric Cantona, Ryan Giggs, Thierry Henry, Roy Keane, Cristiano Ronaldo, Paul Scholes, Alan Shearer, Patrick Vieira na Gianfranco Zola.
Walioorodheshwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora ni 10 tu, huku pakionekana wazi kwamba kuna wanasoka mashuhuri walioachwa. Kwa mfano, Wayne Rooney wa Manchester United na David Beckham aliyewahi kuchezea pia Mashetani Wekundu hao wameshindwa kuingia kwenye mchujo huo.
Ama kwa Chelsea, wapo wawili – Didier Drogba na Frank Lampard, akiwa kiungo pekee aliyefunga magoli 150 katika Ligi Kuu hii. Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard naye pia yupo nje.
Mfaransa Cantona ameteuliwa kuwania tuzo kwenye makundi matano, yakiwa mengi kuliko ilivyo kwa mchezaji mwingine yeyote.
Ukiacha tuzo ya Mchezaji Bora anayowania, Cantona aliyefanikisha timu yake kunyakua kombe mara nne anawania tuzo ya Mfungaji Bora, Nukuu ya Kukumbukwa Zaidi, Ushangiliaji Bora wa Goli na Mshambuliaji Bora. Mshambuliaji wa zamani wa Blackburn na Newcastle, Alan Shearer ameteuliwa kuwania tuzo kwenye makundi manne, wakati washambuliaji wa zamani wa Arsenal, Dennis Bergkamp na Thierry Henry wana makundi matatu kila mmoja.
Matt Le Tissier ndiye mchezaji pekee aliyeteuliwa kuwania tuzo mara mbili kwenye kundi la ‘Goli Bora’.
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anaelekea kukubalika zaidi kwenye kundi la Kocha Bora, ambapo Mskoti huyo anapambanishwa na
Arsene Wenger, Jose Mourinho, Harry Redknapp na David Moyes.

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 10.0/10 (1 vote cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMakala za Michezo

Rais J. M. Kikwete na wanamichezo..

Posted by tanzaniasports.com on February 28th, 2012 | No Comments

Pamoja na kuwa ratiba ya Rais wa nchi yeyote duniani kuwa ngumu kukutana na wale wote wanaopenda kukutana naye, kwa Rais Jakaya Kikwete, ni tofauti kidogo. Alipokuwa London hivi karibuni kwa safari ya kikazi tulipata nafasi mimi na mwenzangu Mariam Komanya kumsalimia Mhe Rais Jakaya Kikwete. Kwa kuonyesha kuwa anatukumbuka, alianza kwa kumuuliza Mariam…”Hujamaliza shule tu…..

Nami akaniuliza vipi Arsenal? kwa kuelewa kuwa mimi nina mapenzi na timu ya Arsenal, na baadaye nikamuuliza Mhe Rais, kama anasikiliza kipindi cha ulimwengu wa soka, kinachotangazwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC toka London, ambapo mimi ni mmoja wa wachambuzi wa masuala ya michezo ya kipindi hicho, akajibu ndio nawasikiliza sana, na kufuatilia masuala ya michezo mnayotangaza.

Kwa hakika tulifarijika sana, na kuona fahari kuwa Mtanzania nje ya nchi yako na rais wako anapata muda wa kujua kile unachokifanya.

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMakala za Michezo

Fact Box

Posted by tanzaniasports.com on January 17th, 2012 | No Comments

Did you know

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: Makala za Michezo

Andy Cole wa Man U aja kusaka vipaji Dar leo

Posted by tanzaniasports.com on June 29th, 2011 | No Comments
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, Andy Cole

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, Andy Cole, anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ajili ya kuzindua mpango maalum wa kuibua vipaji vya soka kwa vijana utakaosimamiwa na klabu hiyo bingwa ya England.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kampuni ya Airtel, ambayo ndiyo iliyoandaa programu hiyo kwa nchi za Afrika ikienda kwa jina la “Nyota wa Soka Wanaoinukia wa Airtel”, kama sehemu ya udhamini wake wa miaka minne kwa klabu hiyo, Andy Cole atazindua mpango huo leo saa 4 asubuhi kwenye shule ya Sekondari ya Makongo.

Mpango huo utashirikisha vijana zaidi ya 500 wa umri wa chini ya miaka 17, ambao wataonyesha vipaji vyao katika michuano itakayoandaliwa kwa ngazi ya mikoa na taifa na kusimamiwa na makocha wa shule za soka za Manchester United.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Leodgar Tenga, alisema kuhusu mpango huo ni jambo kubwa zaidi kupata kutokea katika soka la Tanzania.

“Mipango ya aina hii katika kuibua na kuendelea vipaji vya wanasoka chipukizi ni ufunguo katika kuinua soka la nchi. Na kinachofanya mpango huu wa ‘Nyota wa Soka wa Airtel’ kuwa ‘spesho’ ni ushirikiano wao na Manchester United, moja ya timu kubwa zaidi duniani. Hii inafanya kuwa moja ya mambo bora zaidi yaliyopata kutokea katika soka la Tanzania. Tunajivunia ushirikiano huu na tunaahidi kusapoti mpango huu”.

Akizungumzia sapoti yao katika mpango huo wa “Nyota wa Soka Wanaoinukia wa Airtel”, Mwenyekiti Mtendaji wa Manchester United, David Gill, alisema; “Tunayo furaha kuwasapoti Airtel katika mpango huu na tunawapongeza kwa kusaidia kuibua utajiri wa vipaji vya soka kwa vijana kupitia ‘Airtel Rising Stars’ katika masoko yao 12 barani Afrika. Makocha wa shule ya soka wa Manchester watawafundisha vijana hawa kucheza kwa namna ya Manchester United inavyocheza.”

Fomu za kujisajili kwa ajili ya mpango huo unaotarajiwa kushirikishia vijana zaidi ya 500, utafanyika hadi mwisho wa Julai mwaka huu na zitapatikana katika ofisi za Airtel kote nchini.

Cole aliyetwaa makombe matano kati ya 19 waliyonayo Man U ya Ligi Kuu ya England, aliichezea klabu hiyo kwa misimu 7. Jana alikuwepo nchini Kenya kwa shughuli kama hizo.

CHANZO: NIPASHE
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 1.0/10 (1 vote cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: Makala za Michezo

Mozambique thrash Stars

Posted by tanzaniasports.com on April 25th, 2011 | No Comments
Taifa Stars

Jeremias Sitoe’s double once in each half completely demolished visiting Taifa Stars in a friendly international played at the newly constructed National Stadium here on Saturday night.

Defensive mix up by Stars caused the havoc as striker Sitoe scored all the two goals in similar fashion as the host nation emerged victorious.

Mozambique President Armando Guebuza inaugurated the 40,000 capacity stadium here on the night that saw his boys stealing the show before their home fans.

Fast moving striker Sitoe made full use of defensive mix up by centre back Nadir Haroub and Aggrey Morris to break the stalemate after 19 minutes.

The defensive duo thought Sitoe was off side but the referee was not interested as the hosts registered the opener.

Stars striking trio of Salum Machaku, John Boko and Mwinyi Kazimoto threw overboard glorious opportunities to score following timely clearances by alert Mozambique defenders.

The visitors conceded the second goal under similar circumstances six minutes into the second half to find the tide rising up to their nose.

Stars tried in vain to search of equaliser but time proved unfriendly.

Danish coach Jan Poulsen substituted goalkeeper Shaaban Dihile for Juma Kaseja in the second half to stabilise the defence.

He also replaced Mohamed Banka, Kazimoto and Machaku in favour of Ramadhan Chombo, Mbwana Samata and Julius Mrope in frantic efforts to find an equaliser.

The changes proved effective but goals were elusive as Stars defensive duo of skipper Shadrack Nsajigwa and Haroub were flashed with yellow cards by Swaziland’s referee Simanga Hhleko.

“It’s a poor result but you have played a promising game buoyed by high spirit and determination,” said the Stars coach.

The host side looked aggressive upfront and gave Stars defenders a hectic moment whenever they were in Stars half.

Mozambique are expecting to compete in the All Africa Games to be played here later in September.

Stars coach

Poulsen would make use of one week recess before recalling them for another camp on May 2.

Stars have slightly more than a month before they travel to Bangui for the return leg match of the African Nations Cup qualifier series on June 4.

The Tanzania team has another friendly international against visiting South African national team on May 14, three weeks ahead of their visit to Bangui.

Stars were expected back home by yesterday.

Line-ups:

Stars:

Shaban Dihile/ Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah,Aggrey Morris, Nadir Haroub, Shaabani Nditi,

Mohamed Banka/Ramadhan Chombo, Nurdin Bakari, John Boko, Mwinyi Kazimoto/Mbwana Samata and Salum Machaku/ Julius Mrope.

Mambas: Joao Kampango, Momed Hagi, Eugenio Bila, Eduardo Jumisse/Stelio Ernesto, Carlos Chimomole/Arlindo Cumaio, Sitoe/Danilo Manhonga, Samuel Chapanga/Francisco Muchanga, Francisco Massinga, Almiro Lobo, Celcisio Bonifacio and Zainadine Junior.

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: FeaturedMakala za Michezo

Arsenal’s Arsene Wenger and Samir Nasri charged by Uefa

Posted by tanzaniasports.com on March 9th, 2011 | No Comments
Arsenal manager Arsene Wenger (left) confronts referee Massimo Busacca after the defeat at Barcelona 

Wenger (left) was not happy with referee Busacca

 

Arsenal manager Arsene Wenger and winger Samir Nasri have been charged by Uefa over comments made to the referee after their defeat by Barcelona.

The duo were charged with improper conduct for “inappropriate language”.

Wenger was involved in a furious exchange with Massimo Busacca after Tuesday’s 3-1 loss, which eliminated the Gunners from the Champions League.

The Frenchman was incensed by the decision to show Robin van Persie a second yellow card in the second half.

With the score at 1-1 and Arsenal leading 3-2 on aggregate, Van Persie was given his marching orders in the 56th minute for shooting at goal one second after Busacca had blown the whistle for offside.

Nasri was among a group of Arsenal players who remonstrated with the referee, with Van Persie later claiming he had not heard the whistle because of the noise from the 95,000 crowd.

Wenger confronted Busacca at the final whistle and their angry exchanges continued in the tunnel.

“If you play football at a certain level you cannot understand this decision,” Wenger said. “It killed a promising, fantastic match. If it’s a bad tackle, OK, but frankly it is embarrassing.”

Uefa studied reports from Busacca before charging Wenger and Nasri. The disciplinary case will be heard on 17 March.

After Van Persie’s dismissal, Barca laid siege to the Arsenal goal, taking the lead through Xavi in the 69th minute before a Lionel Messi penalty two minutes later sealed their place in the quarter-finals.

Following their elimination from Europe, Arsenal’s attention now turns to their FA Cup quarter-final away to Manchester United on Saturday.

The Gunners are three points behind leaders United in the Premier League title race with a game in hand.

VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.17_1161]
Rating: 0 (from 0 votes)
Post Tags:
Post Categories: Makala za Michezo
I