in

Ismail Aden Rage ashinda rufaa aachiwa huru

aden-rage.jpg

Rage alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu mwaka 2005 kwa kosa la kuiba zaidi ya Sh3milioni , ikiwa ni fedha taslimu na vifaa vya TFF wakati akiwa katibu mkuu wa chombo hicho kilipokuwa kikijulikana kama FAT.

Hata hivyo, mchezaji huyo wa zamani wa Simba alitoka jela mwaka juzi wakati Rais Benjamin Mkapa alipotoa msamaha kwa wafungwa kabla ya kumaliza kipindi chake cha miaka kumi madarakani.

Lakini Rage alikuwa ameshakata rufaa kupinga hukumu iliyomtupa jela na baada ya kupata msamaha wa rais aliamua kuendeleza kesi hiyo kwa lengo la kujisafisha. Wakati kesi ya rufaa yake ikisubiri kutolewa maamuzi, Rage alitangaza kuachia nafasi yake ya makamu wa pili wa rais wa TFF, ambayo hadi sasa haijajazwa.

Jana majaji wa Mahakama ya Rufaa, Daniel Lubuva, John Mrosso na Salim Mbarouk walibaini kuwa hakukuwa na ushahidi ulioonyesha kuwa Rage aliiba mipira 50 kati ya 600 ambayo anatuhumiwa kuwa aliipokea Uwanja wa Ndege wa Dar es salaam.

“Tumeona kuwa kutokana na kutokuwepo kwa ushahdi kuwa mipira 600 ilipokolewa na Rage, mlalamikaji hakustahili kwa njia yoyote ile kukutwa na kosa la wizi wa mipira 50.

“Tunaamini kuwa kama Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu na Mahakama Kuu zingechambua ushahidi kwa jinsi ambavyo sisi tulifanya, zingeweza kubaini kuwa upande wa mashtaka haukuwe za kutoa ushahidi usio na mashaka,” kwa mujibu wa hukumu ya jopo hilo.

Rage, akionekana mwenye furaha, alisema: “Nina furaha kiasi kwamba siwezi kuwa na maneno sahihi ya kuelezea furaha yangu.”

Rage, ambaye pia alikuwa akielezewa kuwa angewania ubunge wa Jimbo la Tabora kabla ya hukumu hiyo, alikuwa ameshatumikia kifungo kwa miezi mitatu kabla ya kupata msamaha wa rais.

Rage alikuwa anadaiwa kufanya kosa hilo kati ya Februari na Machi 1999. Kesi hiyo ilifunguliwa baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuunda tume ya kuchunguza tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 600 za FAT.

Tume hiyo ilibaini baadaye kuwa ni kiasi cha Sh milioni 160 ndizo zilizokuwa zinaonekana kufujwa na kuwasilisha ripoti kwa mkurugenzi wa taasisi ya kuchunguza makosa ya jinai, DCI, ambayo ilibaini kuwa kiasi cha Sh milioni 40, ikiwa ni fedha na mali za FAT, ndizo zilizoibwa na kuiagiza polisi kufungua mashtaka.

Mbali na Rage, washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo walikuwa mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Muhidin Ndolanga, mhasibu Yonaza Seleki na mfanyabiashara, Specioza Lugazia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Vodacom Tanzania now injects 600m/- in Miss Tanzania 2008

Premier League – Team news: Terry, Lampard doubtful