Latest News
Related News

Vilabu vya Tanzania na Usajili….

MPAKA msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara unakaribia kuanza Simba ndiyo inaweza kuwa timu iliyoingiza fedha nyingi zaidi kutokana na biashara ya kuuza wachezaji nje ya nchi.

Lakini kwa biashara ya kuuza wachezaji ndani ya Tanzania basi tuzo hii kama ingekuwepo ingestahili kwenda kwa klabu ya Mtibwa sugar yenye masikani yake Manungu, Turiani mkoa wa Morogoro.

Klabu hii ya Turiani kwa zaidi ya miaka kumi sasa imekuwa ikiongoza kwa kuuza wachezaji wenye viwango bora kwa timu za hapa hapa nyumbani, hasa kwa klabu kubwa za Simba na Yanga, ambazo haziachi kuiandama klabu hiyo kila kipindi cha usajili kinapofika.

Kwa mfano msimu huu tayari wakata miwa hao wa Turiani imewauza wachezaji wake Shaabani Kadoambaye ni mlinda mlango wake chaguo la kwanza na winga machachari mwenye kasi Jullius Mrope kwa klabu bingwa ya soka nchini Yanga.

Huku mlinzi wake tegemeo Obadia Mungusa na kiungo mchezeshaji Salumu Machaku wakiishia mikononi mwa wekundu wa msimbazi, Simba.Kwa soko la wachezaji la Tanzania kiwango cha juu kabisa kusajiliwa mchezaji hasa akitokea timu kama Mtibwa Sugar inakadiriwa kufikia kwenye shilingi milioni 30 na cha chini ni shilingi milioni 15 hivi.

Tuchukulie kwa mfano wachezaji wote hao wameuzwa kwa shilingi milioni 20 kila mmoja, basi wakata miwa hao watakuwa wamepata shilingi milioni 80, kwa timu ambayo kwa kawaida yake huchukua wachezaji chipukizi na kuwakuza na baadaye kuwauza

Share this to see the whole article

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments